Picha ya Samidoh na Fred Matiang?i Wakati wa Migogoro Kazini Yawasisimua Wakenya

Picha ya Samidoh na mwanasiasa wa upinzani Fred Matiang?i imezua msisimko na tetesi kuhusu uwezekano wa msanii huyo kuingia kwenye siasa

Mjadala huu unakuja baada ya Samidoh kuhamishwa katika idara ya polisi kufuatia kushiriki kwake katika nyimbo za kisiasa, jambo lililoibua malalamiko

Licha ya kushutumiwa kwa kuzembea kazini, Samidoh alijitetea kwa kuwasilisha nyaraka rasmi zilizoonyesha alikuwa likizoni na aliruhusiwa kusafiri hadi Marekani

Picha ya afisa wa polisi aliyeandamwa na lawama, Samidoh, akiwa na mwanasiasa wa upinzani Fred Matiang?i, imewavutia Wakenya, huku baadhi wakidokeza kuwa huenda ni ishara ya mwelekeo wake wa kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027.

Afisa wa polisi mwimbaji Samidoh alikutana na Fred Matiang?i ughaibuni. Picha: Samidoh na Capital FM.

Chanzo: UGC

Mvua ilianza kumnyea Samidoh muda mfupi baada ya kuzuru makazi rasmi ya Naibu Rais Kithure Kindiki huko Karen.

Katika mkutano huo na wasanii wengine kutoka eneo la Mlima Kenya, Samidoh alisema kuwa Rais William Ruto atatawala kwa mihula miwili.

Hata hivyo, muda mfupi baadaye, video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha askari huyo mwimbaji akiwaongoza mashabiki kuimba ?Wantam.?

Kauli hiyo maarufu ilitungwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, ambaye aliondolewa madarakani, kama kauli ya kumpinga Ruto kuwania urais kwa muhula wa pili.

Mabosi wa polisi hawakufurahishwa na kitendo hicho, na Samidoh akahamishwa kutoka Makao Makuu ya Polisi Kanda ya Kati hadi Kitengo cha Kukabiliana na Wizi wa Mifugo huko Gilgil.

Ingawa Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja, alieleza kuwa uhamisho huo ni sehemu ya mabadiliko ya kawaida ya kiutawala, wengi waliuona kama adhabu kwa kujihusisha na siasa.

Lakini mvutano haukuishia hapo. Huduma ya Polisi ya Kitaifa (NPS) ilimshutumu Samidoh kwa kuhepa kazi baada ya kushindwa kuripoti kazini Mei 27 baada ya likizo.

Kulingana na Sheria ya Huduma ya Polisi ya Kitaifa, afisa wa polisi ambaye hashiriki kazi bila ruhusa au sababu halali kwa zaidi ya siku 10, huchukuliwa kuwa amekimbia kazi, isipokuwa ithibitishwe vinginevyo.

Afisa atakayepatikana na hatia ya kukimbia kazi anaweza kufutwa kazi au kufungwa hadi miaka miwili.

Hata hivyo, Samidoh alijibu kwa kuonyesha barua inayoonyesha kuwa alipewa ruhusa ya kusafiri Marekani kwa likizo na alikuwa amepangiwa kurudi kazini tarehe 27 Mei.

Wakati haya yote yakijiri, Samidoh alionekana Marekani akipeana mikono kwa joto na Dkt. Fred Matiang?i, mmoja wa wanasiasa wanaopanga kupinga urais wa Ruto katika uchaguzi ujao.

Samidoh alikuwa amevaa koti, suruali nyeusi, na viatu vya ngozi vya rangi nyeusi, huku Matiang?i akiwa amevaa suruali za kahawia, koti na viatu vya ngozi vya kahawia.

Hali hiyo ilizua tetesi miongoni mwa Wakenya:

Stanleynguli:

?Huenda Samidoh anataka kuwania kiti cha kisiasa.?

mwambatalo_sambataba7_official:

?Hi, cousins.?

njenga.the.og:

?Watatengeneza historia.?

Samidoh anafanya nini Marekani?

Katika habari nyingine, Samidoh anaonekana kufanya ziara ndefu Marekani, ambapo ratiba yake ya tamasha inaendelea hadi mwisho wa Julai, ikionyesha kwamba hatarudi Kenya hivi karibuni.

Ratiba yake ya matamasha ni kama ifuatavyo:

Juni 21 ? Houston

Juni 28 ? Austin

Julai 4 ? Lowell

Julai 5 ? Dallas

Julai 12 ? Seattle

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke