Msichana wa Darasa la Nane Kiambu Atoweka Baada ya Kuonywa Kuhusu Kubeba Juisi Shuleni

Msichana mwenye umri wa miaka 14 alitoweka kutoka nyumbani kwao huko Ruthiruini, kaunti ya Kiambu, mnamo Juni 5 baada ya kurudi kutoka shuleni.

Mamake June Murugi Kimani, Elsie Njambi, aliambia TUKO.co.ke kwamba binti yake aliondoka nyumbani saa moja jioni baada ya kugombewa kidogo kuhusu suala la shule.

Njambi amewaomba Wakenya wamsaidie kumpata binti yake na kutoa taarifa katika kituo cha polisi kilicho karibu au kumpigia simu kupitia 0726708734

Familia moja huko Ruthiruini, kaunti ya Kiambu, inaomba msaada ili kumpata binti yao wa miaka 14, June Murugi Kimani.

June Murugi alitoweka mnamo Alhamisi, Juni 5 saa saba mchana kutoka nyumbani kwoao Kiambu. Picha: Ev Mercy Nungari.

Chanzo: Facebook

Mamake, Elsie Njambi, aliambia TUKO.co.ke kwamba June aliondoka nyumbani mnamo saa moja jioni tarehe 5 Juni baada ya kurudi kutoka Shule ya St Anthony Mugumo, anakosomea.

?Alirudi nyumbani kutoka shule na akaondoka tu, na hajawahi rudi. Ilikuwa jambo dogo ? hakutakiwa kubeba juisi shule, lakini alibeba,? alisema mama aliyekuwa na wasiwasi.

Njambi alieleza kuwa mwalimu wa June alimwambia kwamba wangefahamisha wazazi wake kuhusu suala hilo, na huenda aliogopa na kuamua kutoroka.

Aliongeza kuwa June hakuwafahamisha kuhusu tukio hilo la shule. Alifika tu nyumbani, akabadilisha nguo, na akaondoka muda mfupi baadaye.

?Shule ilikuwa tayari imetupigia simu na kusema alikuwa amebeba juisi. Kwa hivyo alipofika nyumbani, tulimwambia kwamba mwalimu wake alikuwa amepiga simu na kuonya dhidi ya kubeba juisi ? halafu akaondoka,? Njambi alieleza.

June Kimani alikuwa amevaa nini alipotea?

Msichana huyo mdogo alionekana mara ya mwisho akiwa amevaa jezi nyekundu ya Manchester United na kaptula nyekundu. Pia ana braces kwenye meno yake.

Mama yake mwenye huzuni anawaomba yeyote aliyemuona binti yake kuripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu au awasiliane naye moja kwa moja kupitia nambari 0726 708 734 (Elsie Njambi), au amtafute baba yake kupitia 0710 421 348 (Samuel Njoro).

Familia ya Kiambu inamtafuta binti yao aliyetoweka, June Murugi Kimani. Picha: Mary Nduta.

Chanzo: Facebook

Wakenya waombea kurejea salama kwa msichana aliyepotea Kiambu

Wakenya mitandaoni wameonyesha huruma na kutoa sala kwa ajili ya kurejea kwake salama.

Rahab Ndungu:

?Popote ulipo, June, jua tu kwamba wazazi na ndugu zako wanahangaika sana kuhusu mahali ulipo na usalama wako. Tafadhali rudi nyumbani na uwe salama.?

Mary Stephens:

?Rudi nyumbani, binti yangu. Mungu wangu mwema akulinde popote ulipo.?

Jane Nyoike:

?Ni jambo la kuumiza sana kwa familia, hasa kwa kuwa yeye ni msichana mdogo. Mungu amkinge.?

Mercy Hirum:

?Mungu mwema akuongoze dhidi ya mipango yote mibaya ya adui, kwa jina la Yesu. Nguvu za Mungu zikufikie popote ulipo. Maadui wako watawanyike kwa njia saba sasa hivi, kwa jina kuu la Yesu. Msichana mrembo, rudi nyumbani salama kwa jina la Yesu. Umefunikwa kwa damu ya Yesu Kristo. Na kwa wote wanaopitia hali kama hii, Bwana Mungu na aingilie kati. Amina na amina.?

Familia ya Kiambu yaendelea kuwa na wasiwasi baada ya binti yao kutoweka alfajiri

Katika habari nyingine, TUKO.co.ke iliripoti kuwa msichana mwenye umri wa miaka 14 alitoweka kutoka nyumbani kwao eneo la Rironi, kaunti ya Kiambu.

Maureen Wanjiru alitoweka asubuhi ya Mei 21, 2025 baada ya kuamka saa 11 alfajiri kujiandaa kwenda shule.

Mamake aliamka dakika 30 baadaye, na alipomkosa, alidhani alikuwa ameenda shule ? lakini baadaye akaambiwa hakuwa amewasili kamwe.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke