Magazetini: Afisa wa IPOA Alisaidia Kufuta Data Kwenye CCTV Katika Kesi ya Mauaji ya Ojwang'

Jumatatu, Juni 16, magazeti ya kitaifa yaliripoti kuhusu uchunguzi unaoendelea kufuatia mauaji ya kikatili ya bloga na mwalimu Albert Omondi Ojwang.

Magazetini: Mapya Yafichua Afisa wa IPOA Alisaidia Kufuta Data ya CCTV Katika Mauaji ya Ojwang'

Chanzo: Facebook

Magazeti hayo pia yaliangazia matamshi makali ya Rais William Ruto dhidi ya upinzani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.

1. The Standard

Gazeti hili liliripoti kuhusu maendeleo mapya katika mauaji ya kikatili ya bloga Albert Ojwang katika Kituo Kikuu cha Polisi Nairobi.

Mamlaka Huru ya Uangalizi wa Polisi (IPOA) inachunguza maafisa waandamizi kadhaa wa polisi kuhusu nafasi yao katika mauaji ya bloga huyo.

Miongoni mwa wanaochunguzwa ni Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat, OCS Benjamin Talam, Naibu OCS Samuel Ng?ang?a, maafisa sita wa DCI waliomkamata Ojwang, Konstebo Juma Mukwana, OCPD wa Central, afisa wa IPOA, msemaji wa polisi Muchiri Nyagah na fundi wa ICT Kevin Mutisya, anayeshukiwa kufuta picha za CCTV.

Wapelelezi wanahisi kuwa watu wote hao walihusika katika mauaji na mpango wa kuficha ukweli, baada ya polisi kudai awali kuwa Ojwang alijiua.

IPOA inamshuku Konstebo Mukwana kuwa ndiye aliongoza shambulizi dhidi ya Ojwang na pia kuratibu uharibifu wa vifaa vya usalama.

Afisa wa kiufundi wa IPOA pia anashukiwa kusaidia kufuta picha, jambo linalotia mashaka uhuru wa mamlaka hiyo ya uchunguzi inayopaswa kusema ukweli kwa Wakenya kuhusu aliyemuua Ojwang.

2. Taifa Leo

Gazeti hili la Kiswahili liliripoti kuhusu msimamo wa Rais William Ruto kuhusu kuachia madaraka mwaka 2027.

Akihutubia wakazi wa Kaunti ya Kakamega siku ya Jumapili, Juni 15, Ruto alisisitiza kuwa hatawahi kukabidhi madaraka kwa upinzani, akidai kuwa hawana mpango wowote wa maendeleo ya nchi isipokuwa kupalilia ukabila.

Akizungumza katika ibada ya kanisa katika Shule ya Msingi ya Kivaywa, Ruto alihoji nia ya upinzani, akisema hawana ajenda ya wazi kwa Wakenya.

Kulingana na Ruto, upinzani unaoongozwa na naibu wake wa zamani, Rigathi Gachagua, unalenga tu kumuondoa madarakani na haujafikiria kuhusu kuwasaidia Wakenya.

?Hawa watu wengine (upinzani) hawana mpango wowote, msipoteze muda kwao. Hatutakabidhi mamlaka kwa watu wasio na mpango. Mpango wao pekee ni kwamba ?Ruto lazima aondoke.? Hilo litawasaidia Wakenya na nchi vipi?? Ruto aliuliza.

3. The Star

Gazeti hili liliripoti kuhusu kukamatwa kwa raia watatu wanaohusishwa na mauaji ya Ojwang katika Kituo Kikuu cha Polisi Nairobi.

IPOA inaamini raia hao waliandikishwa na maafisa waandamizi wa polisi ili kumtesa bloga huyo hadi kufa.

Watatu hao ? Gin Abwao, Collins Ireri na Brian Mwaniki ? walikamatwa Jumapili, Juni 15, katika oparesheni jijini Nairobi.

Waliambia wapelelezi wa IPOA kwamba walipelekwa katika selo aliyokuwa akizuiliwa Ojwang kwa ajili ya kumtesa ili awape taarifa.

Hii ilikuwa baada ya baadhi ya washukiwa waliokuwa kizuizini kuachiliwa ili kutoa nafasi ya kumweka Ojwang peke yake.

Inadaiwa kuwa mmoja wa maafisa waliokamatwa aliwapa hata rungu maalum walilotumia katika shambulizi hilo.

4. Daily Nation

Gazeti hili liliripoti kuhusu hitilafu za kiufundi katika mfumo mpya wa kuchagua mikondo ya taaluma kwa wanafunzi wa Darasa la Tisa.

Mfumo huo ulivurugika na kuwalazimu walimu katika maeneo ya mashinani kuahirisha shughuli hiyo muhimu kwa kuwa hawakuweza kufikia tovuti.

Changamoto hizo zinajiri huku Wizara ya Elimu ikianza kutoa hamasisho kwa wazazi, walezi na walimu kuhusu jinsi ya kuwaongoza wanafunzi katika mchakato wa mpito wa kuingia shule ya sekondari chini ya mtaala wa CBC.

Katibu Mkuu wa Elimu ya Msingi Prof Julius Bitok alipuuza hitilafu hizo, akiwahimiza wazazi kuwasaidia watoto wao kufanya maamuzi sahihi, akisisitiza kuwa mchakato huo ni rahisi.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke