Albert Ojwang': CCTV Yafichua Kilichotokea Polisi Walipouleta Mwili wa Bloga Hospitali ya Mbagathi

Picha za CCTV zilizopatikana na runinga ya Citizen zimeonyesha wakati Albert Ojwang' alipelekwa katika hospitali ya Mbagathi na gari la polisi

Ojwang' alibebwa akiwa hana uhai nyuma ya Land Cruiser ya polisi na kukimbizwa hospitalini, ambapo alithibitishwa kufariki baadaye

Katika ripoti yao, matabibu wa Mbagathi walibaini kuwa mwili wa Ojwang' ulikuwa wa baridi, bila shughuli za moyo wala kupumua, kuashiria alikuwa tayari amekufa alipoletwa

Picha kutoka kwa kamera za uchunguzi katika Hospitali ya Mbagathi zimeonyesha jinsi polisi walivyochelewa kwa muda kabla ya kumpeleka Albert Ojwang' kwa usaidizi wa kimatibabu.

Albert Ojwang alipelekwa katika Hospitali ya Mbagathi Jumapili alfajiri, Juni 8, akiwa tayari amefariki. Picha: Hospitali ya Mbagathi.

Chanzo: Twitter

Mwanablogu huyo alikuwa amebebwa nyuma ya gari la polisi, ambalo lilifika hospitalini mwendo wa saa 1:35 asubuhi Jumapili, Juni 8, likiegesha kando ya gari la wagonjwa.

Gari hilo lilikuwa na maofisa watatu waliokaa mbele na dereva.

Ojwang' ambaye alikuwa amekata roho alikuwa nyuma peke yake.

Jinsi CCTV ilimnasa Albert Ojwang' katika hospitali ya Mbagathi

Maafisa hao waliovalia sare walishuka na walionekana wakizungumza huku wakifanya harakati kuzunguka eneo la maegesho.

Sekunde chache baada ya kuwasili, wanaonekana wakiingia hospitalini kwa ajili ya kuwashirikisha madaktari wa zamu kabla ya kurejea eneo la maegesho.

Katika eneo la kuegesha magari, maafisa hao wananaswa wakizungumza kwa simu kivyake, kabla ya kuingia ndani ya hospitali saa 1:46 kamili asubuhi, baada ya hapo wanatoka hospitali kuelekea sehemu ya kuegesha magari, safari hii wakiwa na kitanda cheupe cha machela.

Wanaonekana kutokerwa na wakati na uharaka wa dharura iliyopo.

Saa 1:50 asubuhi, maafisa huandaa kitanda cha machela nyuma ya gari, kuondoa mwili.

Kisha wanaitembeza na kuifunika kwa kitambaa cheupe hadi ndani ya hospitali hiyo saa 1:59 asubuhi, huku mlinzi wa hospitali hiyo akiwasaidia kwenye lango kuu la kuingilia.

Maafisa hao walisalia hospitalini kwa takriban dakika 10, huku walionekana wakiutoa mwili huo saa 2:10 asubuhi, hii baada ya madaktari kuthibitisha kuwa Ojwang alikuwa amefariki.

Mmoja wa maafisa hao alikuwa na hati, labda ripoti ya madaktari baada ya kumtathmini Ojwang'.

Waliurudisha mwili ndani ya gari na kuondoka saa 2:15 asubuhi.

Video; hisani

Baadaye katika ripoti yake iliyotupiwa jicho na TUKO.co.ke, afisa wa matibabu mkazi wa Mbagathi, Shah Mitali, alisema Ojwang' alifikishwa hospitalini bila jibu, bila kupumua kwa papo hapo, na hakuna shughuli ya moyo.

Mwili wake wote ulikuwa wa baridi, uso wake ulionekana kuvimba, michubuko mingi kichwani, michubuko kwenye eneo la oksipitali na michubuko kwenye miguu na mikono.

Albert Ojwang aliuawa katika seli ya Kituo cha Polisi ca Central, Nairobi, kabla ya kukimbizwa katika Hospitali ya Mbagathi. Picha: Alberto Januzaj.

Chanzo: Twitter

Unachohitaji kujua kuhusu mauaji ya Albert Ojwang'

Mshawishi wa X mwenye umri wa miaka 31 alifariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi saa chache baada ya kukamatwa nyumbani kwake katika kaunti ya Homa Bay.

Baada ya kifo chake, polisi walidanganya umma kwamba alikufa kutokana na majeraha ya kujipiga baada ya kugonga kichwa chake kwenye ukuta wa seli.

Matokeo ya uchunguzi wa maiti yalionyesha kuwa alishambuliwa na kubanwa shingo yake kama inavyothibitishwa na alama za kubana.

Nani anachunguza mauaji ya Albert Ojwang'?

Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) inachunguza hasa mauaji ya mwanablogu huyo.

Afisa aliyezuiliwa kama kamanda wa Kituo Kikuu cha Polisi, Samson Talam, na Konstebo James Mukhwana, mlinzi ambaye alikuwa zamu wakati Ojwang' alipowekwa ndani.

Kukamatwa kwa marehemu kulifuatia malalamishi dhidi yake ya Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat, ambaye alikuwa amemripoti kwa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kitengo cha Makosa Mabaya kwa madai ya kumkashifu.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke