Edgar Lungu: Aliyekuwa Rais wa Zambia Aliacha Agizo Kali Mrithi Wake Asikaribie Maiti Yake

Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu alifariki Alhamisi, Juni 5, alipokuwa akipokea matibabu maalum nchini Afrika Kusini

Kufuatia kifo chake, ilibainika kuwa Lungu, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 68, aliacha matakwa ambayo yanapaswa kuheshimiwa wakati wa send off yake ya mwisho

Rais huyo wa zamani aliacha maagizo kwamba mrithi wake, Hakainde Hichilema, asiruhusiwe karibu na mwili wake

Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu aliacha maagizo makali ambayo yanapaswa kuheshimiwa wakati wa hafla ya maziko yake.

Hakainde Hichilema haruhusiwi katika mazishi ya Edgar Lungu. Picha: Tony Karumba/Thomas Trutschel

Chanzo: Getty Images

Je, rais wa Zambia ataruhusiwa katika mazishi ya Lungu?

Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Lungu alitoa amri kali kwamba mrithi wake, ambaye ni rais wa sasa wa Zambia, Hakainde Hichilema, asiruhusiwe popote karibu na mwili wake.

TVC iliripoti kuwa hayo ni matukio ya hivi punde katika mzozo mkali kuhusu mipango ya mazishi ya marehemu Lungu.

Serikali ya Zambia ilitarajiwa kusafirisha mwili wa Lungu kutoka Afrika Kusini Jumatano, Juni 11, lakini ilishindwa kufanya hivyo.

Hii ilichangiwa na mzozo wa muda mrefu kati ya familia ya Lungu na chama chake cha siasa, Patriotic Front, kuhusu mipango ya mazishi.

Marehemu Lungu na Hichilema walikuwa mahasimu wa kisiasa kwa kipindi kirefu. Hichilema alimshinda Lungu katika Uchaguzi Mkuu wa 2021 baada ya kushindwa katika majaribio yake matano ya awali.

Akiwahutubia wananchi wa Zambia Alhamisi jioni, Juni 12, rais hakutangaza hadharani matakwa ya mwisho ya Lungu bali alilenga kutoa wito wa amani, upendo na umoja.

Haya yanajiri takriban wiki moja baada ya Lungu kuaga dunia alipokuwa akipatiwa matibabu maalumu nchini Afrika Kusini. Lungu alifariki akiwa na umri wa miaka 68.

Marehemu aliwahi kuwa rais wa Zambia kwa kipindi cha miaka sita kuanzia 2015 hadi 2021. Alichukua wadhifa huo kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Michael Sata.

Alishindwa na Hichilema mnamo 2021, lakini hakukata tamaa. Alirejea mwaka wa 2023, akitafuta kupigania kiti hicho kinachotamaniwa sana.

Hata hivyo, ndoto yake ya kurejea katika kiti cha urais ilikatizwa baada ya mahakama ya kikatiba ya Zambia kutangaza kuwa hana sifa ya kugombea muhula mwingine.

Je, viongozi waliomboleza kifo cha Lungu?

Kufuatia kifo cha Lungu, viongozi mbalimbali akiwemo Rais William Ruto walimlilia kwa heshima za dhati.

Katika salamu za rambirambi kupitia mitandao yake rasmi ya kijamii, Ruto aliihurumia familia ya Lungu na watu wa Zambia.

William Ruto alimuomboleza aliyekuwa rais wa Zambia Edgar Lungu. Picha: William Ruto/Thomas Truschel.

Chanzo: Getty Images

Alimtaja Lungu kuwa kiongozi mpenda maendeleo na bora ambaye aliwahi kuwatumikia Wazambia kwa kujituma na kwa bidii.

Tasila Lungu, ambaye pia anahudumu kama Mbunge nchini Zambia, alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuomboleza kifo cha babake.

Alithibitisha zaidi kuwa babake alikuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini. Aliongeza kuwa safari ya matibabu ya babake ilishughulikiwa kwa faragha na heshima.

Ni ujumbe gani wa mwisho wa Lungu kwa mke wake?

Siku tatu tu kabla ya kifo chake, mwanasiasa huyo wa zamani alikuwa amesherehekea mke wake siku ya kuzaliwa kwake.

Katika ujumbe wa kihisia, Lungu alimwita mkewe kuwa mtoto wake wa kiume na kushukuru kwamba alikuwa msiri wake wa karibu na mwenzi wake wa maisha.

Aidha aliwaomba wanamtandao kujumuika naye kumsherehekea mke wake kipenzi aliyemtaja kuwa mwamba na msiri wake.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke