Video ya Jamaa Akijitetea Baada ya Kudaiwa Kumsukuma Mpwa Wake Kutoka Kwenye Roshani Yaibuka

Video iliibuka ikimuonyesha mwanamume anayedaiwa kumsukuma mpwa wake Amanda Mutheu, kutoka kwenye balcony ya orofa ya tano akijitetea

Amanda alikuwa nyumbani na yaya wake wakati mshukiwa alipomtembelea na inasemekana alizua fujo akiwa amelewa

Licha ya yaya kuwaita majirani, Amanda alipatikana chini kabla ya usaidizi kufika

Nairobi - Video imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanamume anayedaiwa kumsukuma mtoto wa miaka mitano Amanda Mutheu kutoka kwenye roshani ya nyumba ya ghorofa tano.

Mwanamume wa Nairobi akijitetea baada ya kudaiwa kumsukuma mpwa wake kutoka kwenye balcony. Picha: Ann Syovinya/Duncan Ndung'u.

Chanzo: Instagram

Amanda alikuwa nyumbani katika eneo la Jacaranda Estate, Kahawa Magharibi, na yaya wake wakati mshukiwa alipomtembelea na kuripotiwa kusababisha fujo.

Akihisi hatari, yaya alipiga mayowe na kukimbia nje kuwatahadharisha majirani, lakini msaada ulikuja kuchelewa sana wakati malaika alikuwa tayari ameanguka.

Meneja wa makazi ya Jacaranda Gardens, Lilian Gichuhi, alithibitisha kisa hicho katika taarifa, na kusema kuwa mshukiwa alikuwa amelewa sana alipofanya kitendo hicho cha kuchukiza.

Gichuhi pia alithibitisha kuwa maafisa wa polisi waliitwa kwenye eneo la tukio baada ya majirani kumkamata mjombake Amanda, huku wengine wakimkimbiza mtoto huyo hospitalini.

Jambo la kusikitisha ni kwamba mtoto huyo wa miaka mitano aliaga dunia kutokana na majeraha yake alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Mjomba wa Amanda Mutheu ajitetea

Katika video hiyo ambayo sasa inasambaa, mshukiwa, ambaye anaonekana amelewa anaonekana akizuiliwa na wakaazi wa Jacaranda Estate na mlinzi.

Alikuwa na majeraha yanayoonekana usoni mwake, ambayo huenda yalisababishwa na majirani waliokuwa na hasira kufuatia kifo cha Amanda.

Walimhoji kwanini alimsukuma Amanda. Katika utetezi wake, alisisitiza kamwe hakutaka kumdhuru. Alidai Amanda alifurahi kumuona na alionyesha kutoamini shutuma hizo.

"Mutheu ni binti yangu. Ninamtupaje binti yangu? Unaniambia nini? Hapana - nilimtupa mdoli," alisema.

Mwanaume huyo aliendelea kuutaka umati wa watu kummaliza na kumtaja Amanda mara kwa mara huku akisisitiza kuwa ni mtoto wake.

Pia alitaka apelekwe mahakamani na kurejelea kamera za CCTV kwenye roshani, akidai kuwa anajua haki zake.

"Kama kamera zinaonyesha kile kilichotokea, nyinyi mtaaibika," aliongeza.

Wakenya wakasirishwa na kifo cha Amanda

Kisa hicho kimezua hasira za umma mtandaoni, huku wengi wakidai haki kwa Amanda na kulaani vitendo vya mshukiwa.

Forstar Nesh: "Amelewa lakini anasema kuna kamera za CCTV kwenye roshani. Kabla ya kumhukumu na kumpiga, kwa nini usipitie picha?"

Ema Were: "Watu hatari hawapaswi kuruhusiwa kuwa karibu na watoto wetu."

Rose Waithira: "Pombe inapoisha, ukweli utamkumba sana. Kwa kusema alitupa mdoli jamani?"

Senior Generali: "Pombe ikishafifia, hali halisi itatokea. Maisha gerezani pamoja na hatia."

Angeline Wangari: "Ninamjua mnyama huyu. Mara tu unapokuwa na kiasi, utakabiliwa na matokeo na yatakuandama maisha yako yote. Nimekasirika, lakini lengo letu sasa liko kwa dada yako, ambaye hatamwona mtoto wake tena. Umesababisha kiwewe kikubwa. Natumai Mungu atakushughulikia, lakini kwa sasa, kaa gerezani, uwe na kiasi, na usubiri kesi."

Amanda Mutheu alifariki baada ya kudaiwa kusukumwa kutoka kwenye balcony ya ghorofa ya tano jijini Nairobi. Picha: Ann Syovinya.

Chanzo: Facebook

Baba Talisha amfariji mamake Amanda

Katika habari zinazohusiana na hizo, TUKO.co.ke iliripoti kuwa TikToker na mpiga picha Baba Talisha alishiriki rambi rambi zake kwenye mitandao ya kijamii akimfariji mamake Amanda, Ann Syovinya.

Baba Talisha alibainisha kuwa walikuwa kwenye mkutano na Ann wakati tukio hilo lilitokea.

Aliomboleza msichana huyo mdogo na kuombea familia yake nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke