Albert Ojwang': Gumzo la WhatsApp la Maafande Kituo cha Central Lavuja Baada ya Mwenzao Kudaiwa Kuua

Wakenya mtandaoni wanaguswa na uvujaji wa gumzo za WhatsApp zinazodaiwa kutoka kwa kikundi cha ndani cha Kituo Kikuu cha Polisi, kilichohusishwa kufuatia kifo cha Albert Ojwang kizuizini

Ojwang?, mwalimu na mwanablogu, alifariki alipokuwa akizuiliwa katika kituo hicho, na kuzua ghadhabu na uchunguzi nchini kote

Gumzo hizo zilizosambaa kwenye X, zinaonyesha maafisa wakimuonea huruma na kumuunga mkono mwenzao, James Mukhwana, aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo

Afisa wa polisi katika kituo hicho alithibitisha kuwa gumzo hizo ni za kweli, lakini akasema hana uhakika ni nani aliyezivujisha

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamejibu baada ya gumzo za WhatsApp kutoka kwa kundi la Kituo Kikuu cha Polisi kuvuja mtandaoni, huku uchunguzi ukiendelea kuhusu kifo cha Albert Ojwang.

Gumzo kutoka Kituo Kikuu cha Polisi zilionyesha hali ya maofisa hao wakati wa uchunguzi kuhusu kifo cha Albert. Picha: Propesa TV/Mwalimu Alberto.

Chanzo: UGC

Kituo cha polisi chenye makao yake makuu jijini Nairobi kimekuwa papo hapo baada ya kifo cha mwanablogu Ojwang, ambaye alifariki katika kituo hicho, chini ya ulinzi wa wasimamizi wa sheria baada ya kukamatwa wikendi iliyopita.

Gumzo zilizoibuka za WhatsApp kutoka kwa kikundi cha WhatsApp cha kituo cha polisi, ambazo zimekuwa zikisambazwa kwenye X, zilionyesha hali ya maafisa hao baada ya kukamatwa kwa mmoja wao, anayedaiwa kuhusishwa na mauaji ya mwanablogu huyo.

Katika gumzo hizo zilizovuja, baadhi ya juzi usiku, askari hao walimuonea huruma mwenzao ambaye yuko chini ya ulinzi wa polisi, huku baadhi wakiahidi kumwombea.

"Tusimame na mmoja wetu katika maombi na usaidizi. Hapo ndipo upendo kati yetu unajaribiwa," mmoja wao alitoa maoni.

Wengine waliitikia habari za kukamatwa kwa afisa wa polisi James Mukhwana akiwa na emoji za kilio.

"Mungu amsaidie," mwingine alisema.

Mmoja wa maafisa hao pia aliandika ujumbe mrefu, akiwashauri maafisa hao kutowahi kumpokea mshukiwa aliyejeruhiwa kwenye seli bila kufuata utaratibu ufaao.

"Maafisa wa zamu wanapaswa kutembelea seli mara kwa mara, wakionyesha ziara zao kwenye kitabu cha matukio. Usiwatenge wafungwa," aliwaambia wenzake katika kikundi.

Afisa mwingine alitaja kuwa maafisa waliohusika wanahitaji uwakilishi mzuri wa kisheria na dhamana.

TUKO.co.ke pia iliwasiliana na afisa wa polisi aliye kituoni hapo, ambaye alithibitisha kuwa gumzo hizo zilitoka kwa kundi lao, na kuongeza kuwa hakujua ni nani aliyezivujisha.

"Ndiyo, hizo chat ni za kundi letu rasmi la WhatsApp, sijui ni nani aliyezivujisha," alisema bila kutajwa jina.

Gumzo, ambazo zilivujishwa na washawishi wa X, ziko hapa.

Wakenya wazungumzia gumzo la WhatsApp la maafisa wa polisi wa Kituo ca Central

Wakenya waliwajibu kwa maoni yaliyogawanyika, huku wengi wakisema maafisa hao wanapaswa kutoa taarifa zozote zinazoweza kusaidia katika uchunguzi huo.

Hapa kuna baadhi ya maoni:

@justusowaka alisema:

"Bado inasikitisha kwamba wanaomba rehema za Mungu wakati familia inaomboleza mauaji ya mtoto wa pekee na wenzao?"

@Stefan aliandika:

"Hakuna kitu hapa, waache waseme ukweli na wamuokoe mwenzao."

OCS wa Kituo cha Central akamatwa

Haya yanajiri baada ya Afisa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi (OCS) Samson Talam kukamatwa alasiri ya leo kuhusiana na mauaji hayo.

Kukamatwa kwake kunakuja siku chache baada ya kutajwa kuwa mshukiwa wa kifo cha Ojwang, baada ya Mkuu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai, Amin Mohamed, kumtaja kama mtu wa maslahi.

Maseneta na Wakenya walishangaa ni kwa nini Amin alimtenga Talam, ilhali wapelelezi wa DCI walihusika na kukamatwa kwa mwanablogu huyo.

"Yeye ndiye aliyetoa taarifa ya upotoshaji (kwamba Albert aligonga kichwa chake ukutani). Simulizi ya Albert kugonga kichwa chake ukutani ilitoka Kituo Kikuu cha Polisi. Kwa nini mtu atengeneze kitu kama hicho? Ni kwa msingi huo nilisema yeye ni mshukiwa mkuu," Amin alisema.

Polisi James Mukhwana akiwa mahakamani. Picha: TUKO.co.ke.

Chanzo: Original

Askari wa Kituo ca Central akamatwa

Mnamo Alhamisi, Juni 12, polisi Mukhwana alikamatwa kuhusiana na kifo cha mwanablogu huyo.

Mamlaka hiyo ilimtambua mshukiwa mkuu, afisa wa polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi, ambaye alikamatwa na kuzuiliwa Capitol Hill, Nairobi, siku ya Alhamisi.

Siku ya Ijumaa asubuhi, alifikishwa katika Mahakama ya Sheria ya Milimani, akifuatana na timu yake ya utetezi, ikiongozwa na wakili Danstan Omari.

Pia waliokuwepo mahakamani ni IPOA, ambayo iliambia mahakama kwamba ushahidi wote uliokusanywa hadi sasa ulimweka mshukiwa katika eneo la uhalifu.

Shirika hilo liliambia mahakama kuwa Konstebo Mukhwana alitekeleza mauaji hayo pamoja na wengine ambao bado hawajakamatwa.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke