Albert Ojwang: Polisi Anayeshukiwa kwa Mauaji ya Bloga Atumia Familia Yake Rambirambi

James Mukhwana, mshukiwa wa polisi aliyehusishwa na mauaji ya mwanablogu Albert Ojwang, aliwasilisha ujumbe wake wa dhati kwa familia ya marehemu

Akizungumza kupitia kwa mmoja wa mawakili wake wakati wa kikao cha mahakama, anaonekana kudokeza kuelewa machungu ambayo familia hiyo ilikuwa ikipitia

Mukhwana alikamatwa mnamo Alhamisi, Juni 12 na kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Capitol Hill kabla ya kufikishwa kortini

Nairobi: Konstebo wa polisi James Mukhwana, ambaye anahusishwa na mauaji ya mwanablogu Albert Ojwang' alifikishwa mahakamani.

James Mukhana aliwasilisha ujumbe wake wa dhati kwa familia ya Albert Ojwang. Picha: Peter Maruti/Albert Ojwang'

Chanzo: Facebook

Wakati wa kikao cha mahakama, alielezea salamu zake kwa familia ya marehemu.

Mukhwana alikamatwa mnamo Alhamisi, Juni 12 na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Capitol Hill kabla ya kuwasilishwa kortini.

Mshukiwa huyo wa polisi kupitia kwa mmoja wa mawakili wake, Danstan Omari, alichukua fursa hiyo mahakamani kutuma ujumbe wake wa rambirambi kwa familia ya Ojwang.

Mshukiwa huyo wa polisi kupitia kwa mmoja wa mawakili wake, Danstan Omari, alichukua fursa hiyo mahakamani kutuma ujumbe wake wa rambirambi kwa familia ya Ojwang.

"Mteja wangu alikuwa ameniambia nimpe salamu za rambirambi kwa familia iliyofiwa na mpendwa wao, yeye ni binadamu na ni janga kubwa kwa familia yoyote kumpoteza mpendwa wake, kwa niaba ya timu yake ya ulinzi pia tunatoa pole kwa familia ya wafiwa na Mungu awape neema wanapokabiliana na kifo chake cha ghafla," Omari alisema.

Kabla ya hili, risala iliyoelekezwa kwa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) na Mamlaka ya Kuchunguza Utendakazi wa Polisi (IPOA) ilimtaja Mukhwana kama mshukiwa wa mauaji ya mwanablogu huyo.

Hadi alipokamatwa, Mukhwana alikuwa afisa katika Kituo cha Polisi cha Central ambapo mwanablogu Ojwang' alifariki.

Mukhwana alikamatwa na maafisa wa kitengo cha masuala ya ndani na IPOA.

Je, James Mukhwana aliwekwa kizuizini?

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, mahakama iliamua kwamba Mukhwana atazuiliwa kwa siku 21 za ziada kusubiri uchunguzi. Kufuatia maelezo yaliyotolewa mahakamani hapo na IPOA, mawakili wa mshtakiwa na upande wa mashtaka, mahakama hiyo iliomba muda zaidi wa kutoa uamuzi na kupanga Juni 20, tarehe inayofuata ya uamuzi.

Ombi lilifanywa na kuwasilishwa mahakamani na IPOA pamoja na hati ya kiapo ili mahakama kuruhusu kuzuiliwa zaidi kwa mlalamikiwa akisubiri uchunguzi.

Ombi lililotolewa na Abdirahaman Jibril, mkurugenzi msaidizi mwandamizi wa upelelezi wa IPOA, liliipa mahakama sababu kadhaa kwa nini mshukiwa anafaa kusalia rumande hadi uchunguzi ukiendelea.

Maombi hayo yalidai kuwa kuna uwezekano mkubwa mshukiwa alihusika katika kupanga na kutekeleza shambulio la kikatili la kifo cha marehemu katika Kituo cha Polisi cha Central.

Aidha inaeleza kuwa katika uchunguzi wa awali, ilibainika kuwa pamoja na watu wengine kwa ujumla, washtakiwa hao wana uwezekano mkubwa wa kuhusika katika kuficha kwa makusudi kwa kuchezea kanda za CCTV kwenye kituo hicho.

Hati hiyo ya kiapo ilidai kuwa mshtakiwa ana uwezekano wa kuingilia mashahidi na eneo la uhalifu, kumbukumbu za ulinzi na ushahidi mwingine wa kumbukumbu ikiwa itatolewa.

"Hili pia ni suala la umuhimu mkubwa kwa umma na masilahi ya haki na kanuni za sheria zinahitaji kwamba mwombaji azuiliwe ili kuruhusu kukamilika kwa uchunguzi huru na usio na upendeleo na uchunguzi usio na upendeleo na IPOA," maombi mengine mengine yanasema.

Wakili wa mshtakiwa wakati wa kuhojiwa kwa Jibril alibaini kuwa hakuna ushahidi unaounga mkono hati ya kiapo iliyotolewa.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke