Ajuza Auawa Usiku wa Manane na Mvamizi Aliyejificha Ndani ya Nyumba Yake

Bikizee mwenye umri wa miaka 72, Anjeline Kanyi, alipatikana ameuawa katika nyumba yake huko Gatanga, Kaunti ya Murang?a

Muuaji anaaminika kujificha ndani ya nyumba yake kabla ya kumshambulia usiku

Kanyi alipata majeraha ya kudungwa kisu shingoni, kiwiko cha mkono wa kulia na kuthibitishwa kufariki baada ya kukimbizwa hospitalini

Wakenya wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii kumuomboleza mwanamke huyo mzee, huku wengi wakidai kuimarishwa ulinzi kwa wazee

Familia moja huko Gatanga, kaunti ya Murang'a, inaomboleza kifo cha jamaa yao mwenye umri wa miaka 72, ambaye mvamizi asiyejulikana alidaiwa kumuua.

Mwanamke wa Murang'a alivamiwa na mtu anayedaiwa kujificha nyumbani. Picha: Kameme TV.

Chanzo: UGC

Bikizee huyo aliyetambulika kwa jina la Anjeline Kanyi alipatwa na majeraha ya kuchomwa kisu shingoni, kiwiko cha mkono wa kulia asubuhi ya Alhamisi, Juni 12.

Habari zilizosambazwa na Kameme TV zilisema kuwa mtu asiyejulikana anasadikiwa kuwa aliingia nyumbani kwake na kujificha kabla yake kulala.

Mwathiriwa alikimbizwa katika Hospitali ya Kirwara Level Four lakini alithibitishwa kuwa amefariki alipofika.

Polisi wameanza msako wa kumtafuta mshukiwa huyo huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Wakenya waomboleza mwanamke wa Murang'a

Dickson Ndirangu alisema: "Ndio maana naangalia chini ya kitanda changu kabla ya kulala. Apumzike kwa amani."

Elizah Moses aliandika: "Mama mkwe wa dada yangu. Nenda vizuri Wasusana. Ni kama ndoto. Alikuwa mama kipenzi."

Alice Eve "Oh my! Mungu awalinde mama zetu," Christine Wambui "Unaweza kukimbia, lakini huwezi kujificha. Mungu anatazama. Pumzika mama."

Irene Wega Macharia "Wakati mmoja nilimkuta mwanamume akiwa amejikunja mvunguni mwa kitanda changu saa tano usiku. Inatisha."

Mabaki ya mwili wa binadamu yapatikana nyumbani Murang'a

Katika kisa kingine, wanakijiji wa Murang'a walisalia katika mshangao na hofu baada ya fuvu la kichwa cha binadamu kupatikana katika boma la pasta.

Mchungaji huyo alikuwa ameamka mapema na alikuwa akifanya kazi ya ujenzi na wanaume wengine wachache wanusia uvundo

Wakiwa wanatazama huku na kule, walishtuka baada ya kugundua fuvu hilo ambalo walilishuku kuwa lilikuwa limepelekwa kwenye boma hilo na mbwa aliyepotea.

?Chifu msaidizi alifika kwa haraka akiwa na majirani wengine, alianza uchunguzi, na tunataka kujua nini kilitokea, tuliposikia mabaki ya binadamu yamekutwa kwenye boma la mchungaji huyu na tukakimbilia hapa kuona nini kimetokea, tukafika hapa na kugundua ni kichwa kilichokatwa,? alisema jirani mmoja.

Mwanamke wa Murang'a amuokoa mumewe kutokana na jaribio la kutekwa nyara

Kwingineko, hatua ya haraka ya mwanamke wa Murang'a ilimuokoa mumewe dhidi ya wavamizi waliovamia nyumba yao na kujifanya maafisa wa serikali waliotaka kumchukua.

Mfanyibiashara huyo wa Murang?a, Nduati Macharia, alisema watu hao walivamia nyumba yake wakijifanya maafisa wa Mamlaka ya Ushuru ya Kenya waliomshtumu kwa kukwepa kulipa ushuru na kutaka kumchukua.

?Walipovamia nyumba hiyo walimkuta mke wangu, mwanangu na mfanyakazi wangu na kuniomba, ndipo nilipomuona mmoja akimpiga mtoto wangu kofi sikuweza kuvumilia nikaenda kuangalia ni akina nani,? anasimulia.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke