Eric Omondi Achangisha KSh 750,000 kwa Saa Chache Kumsaidia Mzee wa Gatundu Aliyempoteza Mjukuu

Wakenya wameitikia kwa ukarimu wito wa Eric Omondi uliojaa hisia, wakichangisha pesa kumsaidia babu mmoja wa Gatundu aliyempoteza mjukuu wake katika hali ya kusikitisha

Video iliyosambaa mitandaoni ilimuonyesha James Muiruri akiwa na majonzi akiwakabili wahudumu wa hospitali, akidai uzembe wa kitabibu na kusema kuwa dereva wa ambulansi alichelewesha msaada

Familia ilisema kuwa mtoto alifariki baada ya kunyimwa huduma kwa wakati kutokana na ucheleweshaji, ukosefu wa bima ya afya, na mgomo wa wahudumu wa afya

Wakenya wamesikia wito wa Eric Omondi wa kusaidia mzee wa Gatundu aliyempoteza mjukuu wake, akilaumu tukio hilo kwa uzembe wa madaktari.

Eric Omondi aliwaomba Wakenya kuchangisha fedha kwa ajili ya familia ya James Muiruri. Picha: Eric Omondi.

Chanzo: Instagram

Video yenye hisia kali ilisambaa mtandaoni, ikimuonesha James Muiruri aliyekuwa na huzuni mwingi katika tukio la kusikitisha na wafanyakazi wa Hospitali ya Igegania Level 4.

Kwanini dereva wa ambulansi hakumsaidia babu wa Gatundu?

Katika video hiyo, Muiruri alionekana akiwa katika mzozo wa vurugu huku akiwa amembeba mjukuu wake aliyefariki, akiwalaumu wahudumu wa hospitali, akiwemo mlinzi, kwa kushindwa kuchukua hatua kwa haraka kuokoa maisha ya mtoto huyo.

Video hiyo ilisambaa kwa kasi mitandaoni na kumfanya mchekeshaji na mwanaharakati Eric Omondi kuingilia kati. Akiwa ameguswa sana na tukio hilo, Eric alimpigia simu Muiruri kisha baadaye akamtembelea nyumbani kwake Gatundu ili kumpa faraja.

Katika ziara hiyo, Eric pia alikutana na mama wa mtoto huyo, ambaye ni binti ya Muiruri, aliyefafanua kuwa mtoto alikuwa na miezi 11 pekee na alikuwa amepewa jina la babu yake, jambo lililoongeza majonzi ya familia hiyo.

Eric, akiwa na nia ya kusaidia, aliwahimiza Wakenya kuchangia chochote walichokuwa nacho kusaidia familia hiyo katika wakati huo mgumu, na akachapisha nambari ya simu (0725910162) kwa yeyote aliyependa kutoa msaada.

Saa chache baada ya ombi hilo, Eric alitoa taarifa mpya akieleza kuwa Wakenya walikuwa wamechangisha kiasi kikubwa cha pesa.

Katika video hiyo, Muiruri alieleza kuwa mtoto hakulazwa hospitalini kwa sababu hakuwa amesajiliwa kwenye Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA).

?Nilimpigia mtu na akanambia nisajili SHA na pia nilipie faini. Nilituma KSh 3,600.?

Muiruri alisema madaktari walimweleza kuwa mchakato wa kumlaza mtoto ulikuwa umechelewa kwa sababu wahudumu wa afya walikuwa kwenye mgomo. Kisha akaomba ambulansi impeleke mtoto katika hospitali nyingine.

?Alikuwa amewekewa oksijeni kwa sababu alikuwa na shida ya kupumua. Lakini dereva wa ambulansi alisema alikuwa anakunywa chai na hakuwa amepokea maagizo yoyote ya kunisaidia.?

Muiruri alisema alianza kupiga kelele baada ya kuona hali ya mtoto ikibadilika, ndipo mtoto akafariki.

?Tayari tuko kwa KSh 750k. Mungu awabariki wote waliotuma chochote. Msikose kitu kamwe! Mfumo umetuumiza. Mfumo hutuumiza, lakini siku njema zinakuja.?

Aliendelea kuwataka Wakenya waendelee kusaidia familia hiyo kifedha.

Eric Omondi alivyosaidia bibi wa Homa Bay

Kwingineko, Eric hivi karibuni alitembelea Consolata Aoko Oduya, bibi ambaye alivuta hisia za umma baada ya kutoa kuku ili kulipia karo ya wajukuu zake.

Eric Omondi aliguswa na upendo wa Consolata Aoko Oduya kwa wajukuu zake. Picha: Eric Omondi na Kabz Nyar Kisii.

Chanzo: Instagram

Akiwa ameguswa na moyo wake wa kujitolea, mchekeshaji huyo aliahidi kufadhili elimu ya watoto hao hadi chuo kikuu na pia kusaidia kuanzisha biashara ndogo kwa bibi huyo.

Aliwafuatana na watoto hao hadi shuleni na kuhamasisha Wakenya wengine kumsaidia bibi huyo mwenye kujitolea.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke