Kiambu: Simanzi Baada ya Dada Wawili Kufariki Pamoja Wakivuka Barabara Gitaru

Kamanda wa Polisi eneo la Kikuyu, Joseph Ndege, alieleza kwa uchungu kuwa dada wawili walifariki kwenye ajali ya barabarani eneo la Gitaru, kaunti ya Kiambu

Wawili hao walikuwa wakijaribu kuvuka Barabara Kuu ya Nairobi-Nakuru katika eneo lisiloruhusiwa watu kuvuka wakati ajali hiyo ilipotokea

Ndege alibainisha kuwa miundombinu ya barabara hiyo bado inajengwa, na akawaomba madereva na watembea kwa miguu kuwa waangalifu wanapoitumia

Wingu la huzuni na majonzi lilitanda miongoni mwa wakazi wa Gitaru, kaunti ya Kiambu, kufuatia tukio hilo la kusikitisha.

Msongamano mkubwa wa magari kwenye Barabara kuu ya Nairobi-Nakuru. Picha: Mtaa Wangu.

Chanzo: UGC

Dada hao wawili walipoteza maisha yao baada ya kuripotiwa kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani.

Ni lini dada wa Kiambu walifariki katika ajali ya barabarani?

Waligongwa na lori katika Barabara Kuu ya Nairobi?Nakuru walipokuwa wakijaribu kuvuka barabara siku ya Ijumaa, Mei 30.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Kikuyu, Joseph Ndege, alithibitisha tukio hilo huku akitoa maelezo zaidi kuhusu mkasa huo.

Alisema kuwa dada hao walikuwa wakivuka barabara katika eneo lisiloidhinishwa, jambo ambalo amesema limechangia ongezeko la ajali kwenye barabara hiyo yenye shughuli nyingi.

"Barabara hii bado inajengwa, na kwa sababu hiyo, ishara na alama bado hazijawekwa. Tahadhari kuu zinazohitajika?alama za barabarani na vizuizi vya kutenganisha njia?bado hazipo," alisema Ndege.

Kilio cha Joseph Ndege kwa madereva na wapita njia

Aliwahimiza watumiaji wote wa barabara, hasa watembea kwa miguu na madereva, kuwa waangalifu zaidi wanapotumia barabara hiyo ambayo bado haijakamilika.

Kwa kuwa miundomsingi bado haijakamilika, afisa huyo alitoa wito kwa watumiaji wote wa barabara kuwa waangalifu ili kuepusha ajali na kupunguza vifo.

Ndege aliongeza kuwa polisi wa trafiki wameweka mikakati ya kuboresha usalama na kuokoa maisha.

"Tumewapeleka maafisa wetu wa trafiki katika eneo hilo. Tunajaribu kuwaelekeza watembea kwa miguu jinsi ya kuvuka kwa usalama," aliongeza.

Wakenya watoa maoni kuhusu ajali ya barabara ya Nairobi-Nakuru

Tukio hilo la kusikitisha liligusa mioyo ya wengi mitandaoni, huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakimiminika kwenye sehemu ya maoni kuonyesha huzuni yao:

Nancy Madanji:

"Barabara hiyo haina daraja la waenda kwa miguu wala alama ya kuvuka barabara (zebra crossing). Serikali inapaswa kuchukua hatua kwa sababu kuna shule ya umma karibu, na wanafunzi huvuka barabara hiyo kila siku."

Charity Wairima:

"Mungu wetu ni mwenye rehema na mwaminifu. Tuombee nchi yetu. Dada hao wapumzike kwa amani."

Ruth Mukunga:

"Sijawahi kuona daraja la wapita kwa miguu katika eneo hilo. Karibu na alama ya zebra crossing, watu mara nyingi huvuka kwa kupenyeza kati ya vizuizi."

Faith Chepkoech:

"Rambirambi zangu za dhati kwa familia. Pumzikeni kwa amani dada zetu."

Sammy Shichenga:

"Baba na mama hawatapata chakula cha jioni leo na binti zao. Inasikitisha sana ????. Wapumzike kwa amani."

Njugush Wa Gas:

"Namlaumu Ruto. Dada hao walipaswa kuwa kanisani wakifanya mazoezi. Wanateseka kwa sababu ya hali ngumu ya uchumi inayosababishwa na utawala wa Ruto."

Ajali nyingine ya barabarani kwenye Barabara ya Nairobi-Mombasa

Katika tukio lingine la kusikitisha la ajali ya barabarani, ajali ya kutisha iliyohusisha malori matatu ilitokea kwenye Barabara Kuu ya Nairobi?Mombasa na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

Ajali hiyo ilisababisha hali ya sintofahamu, huku madereva na abiria wakikwama kwa muda mrefu.

Mtu mmoja alipoteza maisha, na mwingine alijeruhiwa vibaya.

Wahudumu wa dharura walifika katika eneo la tukio mara moja kushughulikia hali hiyo.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke