George Ruto: Mwanamitindo Aliyepigwa Picha na Mwanawe Rais Huko Bali Avunja Ukimya

Mwanamke Mkenya, Sheila Mutundi, amezungumza baada ya picha yake akiwa na George Ruto nchini Bali kusambaa mitandaoni

Alifafanua kuwa kukutana kwao kulikuwa kwa bahati tu, na aliomba kupiga picha naye kwa sababu ya hadhi yake

Sheila pia alieleza kuwa mashambulizi ya mtandaoni yaliyofuata yalimuathiri sana, kihisia na kiakili, na akawasihi Wakenya waendelee kuwa na matumaini na mshikamano

Kisura Mkenya aliyeonekana na George Ruto huko Bali amezungumza.

Sheila Mutundi alizungumza kuhusu kukutana na George Ruto. Picha: Sheila Mutundi.

Chanzo: Instagram

George alijikuta katikati ya gumzo mtandaoni baada ya kuonekana na mwanamitindo wa Instagram, Sheila Mutundi.

Wapekuzi wa mitandao waligundua haraka kuwa Sheila alikuwa tayari amewahi kutembelea kisiwa hicho cha kitropiki, na safari zake za awali zikiwa zimewekwa kwenye sehemu ya highlights ya Instagram yake, ishara ya upendo wake kwa eneo hilo.

Gumzo kuhusu picha hiyo lilimlazimu Sheila kujitokeza na kujieleza, huku akiwashutumu wanamtandao kwa kumshambulia.

Alifafanua uhusiano wake na George na kueleza jinsi walivyokutana na mwana wa rais nchini Indonesia.

?Mimi na Alexander tulikutana tu na George bila kutarajia hapa Bali. Kwa kuwa yeye ni mwanawe rais, niliomba kupiga naye picha. George ni mtu mkarimu, mnyenyekevu, na mtulivu sana ambaye alikuwa amevaa Crocs. Sichumbiani na mwanaume yeyote kati yao,? alisema.

Sheila alikiri kuwa kukutana na George ilikuwa jambo kubwa kwake:

?Picha yangu na George ina maana sana kwangu. Nilivyokua, usingeweza hata kufikiria kukutana na mwana wa rais, sembuse kuwa Bali. Ni kumbukumbu niliyotaka kushiriki na familia na marafiki. Nilibughudhiwa kwa kupiga picha na George. Nilihisi kukataliwa na kudhalilishwa na watu wangu. Ilinigharimu kiakili, kihisia, na hata kifedha kwa kuwa sasa napitia tiba ya kisaikolojia (therapy) ambayo si rahisi kugharamia.?

Kipusa huyo pia alieleza kujiamini kwake kwa sura na umbo lake:

?Paji langu, mifupa yangu, na shingo yangu ndogo hunifanya nionekane mrembo sana! Naheshimu maoni yenu kuhusu muonekano wangu, lakini mimi ni mrembo haswa.?

Sheila alituma ujumbe wa moyo kwa Wakenya, akieleza kuelewa hali ngumu wanazopitia chini ya serikali ya Ruto:

?Kwa Wakenya wenzangu, iwapo mtaona hii, najua nawapenda. Nimezaliwa Kenya na ninaelewa kile wengi mnapitia. Baba yangu alikuwa mlinzi na mama yangu aliuza pombe ya kienyeji. Nilipitia maisha magumu sana, nikakosa kila kitu karibu kila siku. Lakini hatufai kuacha kupigania haki yetu. Kiongozi yeyote ambaye hafanyi haki kwa watu lazima aondoke.?

George Ruto anasomea nini?

Rais William Ruto hivi majuzi alieleza fahari yake kuhusu mwanawe, George, ambaye anapendelea sana maswala ya mchezo wa kandanda.

Akiwahutubia vijana wa timu ya taifa ya U-20 ya Kenya, Rising Stars, wakati wa hafla ya kuwaaga kabla ya kwenda mashindano ya AFCON nchini Misri, Ruto alisema kuwa George anasomea shahada ya uzamili katika usimamizi wa michezo (sports management).

?George ana mapenzi makubwa na mambo ya michezo, na hilo limenichochea kuwekeza zaidi kwenye maendeleo ya michezo nchini,? alisema rais.

Alitia moyo timu hiyo kabla ya mashindano hayo na kuahidi kuwa, ikiwa Kenya itafuzu hadi fainali, atahudhuria mechi hiyo kama ishara ya kujitolea kwake kukuza vipaji vya vijana kupitia michezo.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke