Mke wa Kwanza wa Karangu Muraya, Triza, Awachanganya Mashabiki baada ya Kusema Yuko Singo

Triza Njeri amekuwa akipata kazi za matangazo kila kona hivi majuzi, na mashabiki wake wanafurahia mafanikio yake

Mama huyo wa watoto watatu alichapisha ujumbe unaodokeza kuwa yuko single, jambo lililowachanganya mashabiki

Chapisho la mke wa kwanza wa Karangu Muraya linakuja wiki chache baada ya Muraya kumzawadia gari kufuatia maridhiano yao

Mke wa kwanza wa Karangu Muraya, Triza Njeri, amewachekesha mashabiki baada ya kudai kuwa yuko single.

Karangu Muraya na Triza Njeri wamekuwa pamoja kwa miaka 13 na wamebarikiwa kupata watoto watatu. Picha: Karangu Muraya, Triza Mamake Muraya.

Chanzo: Facebook

Je, Karangu Muraya na Triza wamerudiana?

Mama wa watoto watatu amekuwa akiunda maudhui ya kuvutia mashabiki wake. Triza alichapisha video akicheza ngoma ya Kikuyu, akionyesha mitindo yake ya kucheza.

Kwenye video hiyo, Triza alikuwa amevaa blauzi ya waridi, sketi ya kijani kibichi, viatu virefu vyeupe na kitambaa cha kichwa cha rangi ya buluu ya angani.

"Nipo sokoni, upande wa Marikiti????????????????????????????."

Katika lugha ya sheng, mtu anaposema ako soko, humaanisha hana mpenzi. Chapisho la Triza liliwaacha mashabiki wakijiuliza kama amemuacha mumewe kabisa.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya mashabiki:

Ruth Kariuki Karuth:

"Napenda vile ulijitambua, ukatengeneza taji lako ????????????????."

Anita Alex:

"Enda hapo kwa vitunguu za red ????????????."

Njeri Mungai:

"Bora usiende side ya avocado, utafinywafinywa."

Kadadi official:

"Soko nayo kurudi ni kawaida."

Charity Muchiri:

"Huyu alipona eneo la uhalifu????."

Patricia Mwangi:

"Marikiti upande gani? Kwa waru, vitunguu ama kabeji? ????"

Steve Mwihia:

"Anapenda drama."

Wairimu Kariuki:

"Sisi tuliingia soko miaka 10 iliyopita na bado hatujapata wateja, awache kiherehere."

Rukii Khadija:

"Anataka kutrend tena."

Karangu Muraya aonyesha upendo kwa Triza

Hivi majuzi, Karangu alieleza upendo wake kwa mke wake wa kwanza, akiapa kumuunga mkono katika kazi yake ya muziki, miezi kadhaa baada ya Triza kudai kuwa hawako pamoja tena.

Karangu alichapisha ujumbe wa kuutangaza wimbo mpya wa Triza, na shabiki mmoja akacomment akisema angekuwa amemwita ex wake.

Baba huyo wa watoto watatu alimsahihisha shabiki huyo, akisisitiza kuwa bado wameoana na Triza.

Je, Karangu Muraya aliachana na Carol Kim?

Mwezi wa Januari, Karangu alimtambulisha mke wake wa pili kwenye mitandao, jambo lililomuumiza Triza.

Karangu na Carol Kim waliendelea kushiriki hadithi yao ya mapenzi mtandaoni, hali iliyowaacha wengi wakiwa na wivu.

Hivi majuzi, video ya Carol akilia ilisambaa mtandaoni huku uvumi ukienea kwamba ameachana na Samidoh.

Hata hivyo, mama huyo wa mtoto mmoja alikanusha madai hayo, akieleza kuwa video hiyo ilikuwa ya mwaka 2020 wakati alifanya changamoto ya TikTok.

Triza Njeri hivi majuzi alihamia katika nyumba yake. Picha: Triza Mamake Muraya.

Chanzo: Facebook

Je, Triza anaishi na Karangu Muraya?

Hivi karibuni, Triza alitangaza kuwa amehama na kuingia katika nyumba mpya.

Mama huyo wa watoto watatu alishiriki video akionyesha makochi mapya ya kuvutia. Alimshukuru mmiliki wa Modern Pacific Furniture, Gibson Murage, ambaye pia ni bosi wake mpya, kwa fanicha hiyo.

Karangu pia alijiunga na mashabiki kumpongeza mke wake, akimtakia mafanikio maishani.

Triza alikuwa akiishi na rafiki yake wa karibu Tata Essy kabla ya kuhamia nyumba yake.

Essy alieleza kuwa Triza aliondoka nyumbani kwake bila taarifa, baada ya uzinduzi wa albamu yake kufanikiwa, ambapo alipokea zaidi ya KSh 1 milioni kwa michango.

Alihadithia jinsi alivyomsaidia Triza, lakini akaja kusalitiwa naye.

Kwa sasa, haijathibitishwa waziwazi kama Triza na Karangu wamerudiana, lakini ishara zinaonyesha bado kuna uhusiano wa karibu unaoendelea kwa namna fulani.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke