Magazetini: Mwanafunzi wa Chuo Apatikana Amefariki Siku Chache Baada ya Kuzozana na Walinzi

Jumatatu, Juni 2, magazeti ya kitaifa yaliripoti kwa mapana kuhusu sherehe za Madaraka Day za mwaka wa 62 zilizofanyika katika kaunti ya Homa Bay.

Magazetini: Mwanafunzi wa Chuo Apatikana Amefariki Siku Chache Baada ya Kuzozana na Walinzi

Chanzo: UGC

Magazeti hayo pia yaliripoti kuhusu maandamano yaliyozuka kufuatia kukamatwa kwa mwanaharakati wa kupinga Mswada wa Fedha wa 2025, Rose Njeri.

Daily Nation

Gazeti hili liliripoti kuhusu hoja kuu zilizotolewa na Rais William Ruto wakati wa sherehe za Madaraka Day za mwaka wa 62.

Akizungumza katika Uwanja wa Raila Odinga siku ya Jumapili, Juni 1, Ruto alielezea mafanikio na mageuzi yaliyotekelezwa na serikali yake ya Kenya Kwanza.

Rais Ruto pia alizindua mfumo mpya wa malipo kwa ajili ya Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA).

Alitangaza mpango wa Lipa Pole Pole ili kurahisisha michango ya bima ya SHA kwa Wakenya wanaofanya kazi katika sekta isiyo rasmi.

Kupitia mpango huu mpya, wananchi wanaweza kulipa ada zao za kila mwaka kwa awamu au kupitia njia rahisi zaidi ya malipo.

?Ili kushughulikia changamoto sugu kama vile ucheleweshaji wa michango ya bima miongoni mwa wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi, tunazindua suluhisho bunifu na jumuishi la malipo liitwalo LIPA SHA POLE POLE. Mpango huu unawawezesha Wakenya kulipa michango yao ya kila mwaka ya SHA kwa awamu rahisi?iwe ni kila mwezi, kila wiki, au hata kila siku?kulingana na uwezo wao wa kifedha,? Ruto alitangaza.

Rais William Ruto akizungumza wakati wa sherehe za Madaraka Day. Picha: William Ruto.

Chanzo: Facebook

The Star

Gazeti hili liliripoti kuhusu kupatikana kwa mwili wa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Kenya Utalii, Nairobi.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 20 alipatikana akiwa amefariki katika moja ya mabweni ya chuo hicho siku ya Ijumaa, Mei 30, siku chache baada ya kuripotiwa kutoweka.

Mwili wake uliokuwa umeanza kuoza ulipatikana katika chumba kilichokuwa kimefungwa kutoka ndani.

Ugunduzi huu ulifuatia malalamiko kutoka kwa wanafunzi kuhusu harufu kali iliyokuwa ikitoka katika chumba hicho kilicho katika ghorofa ya tatu.

Kulingana na wanafunzi, marehemu alikuwa amekuwa na mzozo na walinzi wa chuo hicho katika lango kuu siku chache zilizopita.

Video ya tukio hilo inadaiwa kusambazwa katika makundi ya WhatsApp kabla ya mwili wake kupatikana.

Kupatikana kwa mwili huo kuliibua maandamano katika chuo hicho huku wanafunzi wakidai kuwa mwenzao aliuawa.

The Standard

Gazeti hili liliripoti kuhusu maandamano yanayoendelea kufuatia kukamatwa kwa mtaalamu wa programu za kompyuta na mwanaharakati Rose Njeri.

Njeri alikamatwa Ijumaa, Mei 30, huko South B kwa madai ya kubuni tovuti ya kurahisisha upinzani wa umma dhidi ya Mswada wa Fedha wa 2025.

Kuzuiliwa kwake kumezua malalamiko makubwa mitandaoni huku wanaharakati wa haki za binadamu wakilalamikia kutoshikiliwa kwake kwa dhamana wala kufunguliwa mashtaka rasmi.

Wanasheria wamelaani kukamatwa kwake wakisema ni mbinu ya kuwatisha Rose na wale wengine wanaopinga Mswada huo wa Fedha.

Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK) kikiongozwa na Rais wake Faith Odhiambo kimeeleza masikitiko yao kuhusu ugumu wa kupata ruhusa ya kumtembelea Rose ili kumpa msaada.

?Juhudi zote za kuhakikisha anapewa dhamana ya polisi zimekwamishwa na maafisa wanaosimamia kesi hiyo, ambao hawajajibu ombi la mawakili,? Odhiambo alisema katika taarifa.

Taifa Leo

Gazeti hili liliripoti kuhusu hatua ya viongozi wa upinzani kukosa kuhudhuria sherehe za Madaraka Day za mwaka wa 62.

Makamu wa Rais wa zamani Rigathi Gachagua alihudhuria ibada ya kanisa katika kaunti ya Kiambu kisha akaandaa mikutano kadhaa ya barabarani.

Kiongozi wa chama cha Wiper Democratic Movement, Kalonzo Musyoka, pia hakuhudhuria sherehe yoyote ya hadhara bali alichapisha ujumbe wake kwa Wakenya kupitia mitandao ya kijamii.

Huko Trans Nzoia, Gavana George Natembeya pia alikosa kuhudhuria sherehe hizo za kitaifa, akieleza kuwa amevunjika moyo na hali ya nchi.

?Kwa sasa sina cheo chochote cha mamlaka, kwa hivyo kwa nini nihudhurie sherehe za mamlaka? Umaskini unaokithiri ni aina mpya ya ukoloni. Tumekuwa tukijidanganya, na nitafikiria kwa kina kama nitahudhuria sherehe kama hizi siku zijazo,? alisema Natembeya.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke