William Ruto Awavutia Wengi kwa Hotuba ya Kifasaha kwa Lugha ya Kidhuluo:"Tunachapa Kazi Bila Break"

Rais Ruto alinukuu wimbo wa Prince Indah uitwao Osiepe ili kusisitiza kujitolea kwake kufanya kazi bila kukatizwa licha ya mvutano wa kisiasa

Rais aliwavutia wengi kwa hotuba yake ya Kidhuluo kwa ufasaha wakati wa sherehe za 62 za Madaraka Day

Watu mitandaoni walishangazwa na ufasaha wa Ruto katika lugha ya Kidholuo, wengi wakionyesha kuvutiwa na juhudi zake za kuungana na wenyeji wa Nyanza

Rais William Ruto aliwashangaza Wakenya wengi kwa furaha baada ya kutoa sehemu ya hotuba yake ya Madaraka Day kwa Kidhuluo fasaha.

William Ruto aliwashangaza wengi baada ya kuzungumza Kidhuluo kwa ufasaha katika sherehe za 62 za Madaraka Day. Picha: William Ruto.

Chanzo: Facebook

Rais wa Jamhuri aliwavutia waliohudhuria sherehe za Madaraka Day za mwaka wa 62 zilizofanyika katika Uwanja wa Raila Odinga, kaunti ya Homa Bay, kwa kuzungumza kwa kujiamini kutoka kwenye mimbari.

Ruto alinukuu maneno kutoka kwa wimbo maarufu wa msanii wa Kijaluo Prince Indah uitwao Osiepe, jambo lililosababisha umati kulipuka kwa makofi na shangwe.

?Sisi hatuna maneno. Sisi tunapiga tu kazi. Sisi hatuna wasiwasi,? alisema kwa Kijaluo, akikariri mistari kuhusu kujitolea na kutoyumbishwa.

Rais alitumia fursa hiyo kuimarisha msimamo wa serikali yake kuwa wanaendelea kufanya kazi licha ya kelele na ukosoaji wa kisiasa unaoongezeka.

?Hatuna wasiwasi, hatuna midomo mingi, tunachapa kazi. Ile kazi bila break ndiyo tunachapa. Tuendelee ama tusiendelee?? aliuliza, na umati ukajibu kwa shangwe.

Ufasaha wake katika lugha ya Kijaluo uliwavutia sana wakazi, kwani ulikuwa wakati wa pekee ambapo rais alionekana kuungana moja kwa moja na watu.

Kwa miaka mingi, Rais Ruto amejijengea sifa ya kuzungumza lugha mbalimbali za wenyeji, ambapo tayari amewahi kuhutubia watu kwa Kiluhya, Kikuyu, na hata Kisomali katika ziara zake.

Baadhi ya maoni ya mitandaoni yalikuwa:

Doris Dorice: "Huyu tumezoea, hakuna lugha hajui sasa 'wows Kenyans' ni kawaida tu."

Jonathan Masila Mutuku: "Tunataka kazi si siasa Mheshimiwa Rais."

Muiruri Harun: "Alikuwa anasoma hiyo speech ya Dholuo kwa karatasi. Tulitazama my friend."

Jack Mwai: "Ukiangalia Kijaluo anazungumza vizuri lakini Kikuyu anameza ulimi."

T?r? A M?mbi: "Aliitumia usiku mzima kuikariri hiyo lugha ya Kijaluo unayosema."

William Ruto aliongoza sherehe ya 62 ya Madaraka Day katika uwanja wa Raila Odinga huko Homa Bay.

Chanzo: Twitter

Rachel Ruto alivaa nini kwenye Madaraka Day?

Katika sherehe hizo hizo, Mama wa Taifa Rachel Ruto alivutia macho kwa vazi lenye maana ya kizalendo lililoakisi rangi za bendera ya Kenya.

Nguo yake ya urefu wa kifundo cha mguu ilikuwa na rangi ya kijani kama rangi kuu, sehemu nyekundu ikianzia begani kulia kushuka mbele, na bega la kushoto likiwa na rangi nyeusi.

Mistari midogo meupe ilipita kwenye sehemu nyekundu na kukamilisha muonekano wa bendera ya taifa.

Aliambatana na mkoba wa kisasa na nywele zake fupi alizozoeleka nazo.

Muonekano wake ulitoa taswira ya ustadi, uzuri wa ndani na heshima iliyolingana na siku hiyo ya kitaifa.

Rais Ruto naye alivalia suti ya buluu iliyomkaa vyema, shati jeupe safi, na tai nyekundu kali ? vazi lililoonesha mamlaka na uzuri wa heshima ya taifa.

Joyce Kindiki alivaa nini kwenye Madaraka Day?

Joyce Kindiki mkee jaibu rais alivaa gauni refu la lace ya rangi ya maroon, alitokelezea na wigi fupi la blonde, viatu virefu vya block vya rangi ya fedha, na mkufu mweupe mkubwa kama kiambatisho.

Naibu Rais, Kithure Kindiki, alivalia suti ya buluu ya giza, shati jeupe na tai ya maroon ? muonekano wao ulikuwa wa kupendeza na waliambatana kwa mazungumzo mepesi walipokuwa wakitembea pamoja.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke