Bromance: Picha 7 za Ruto na Raila Zikionyesha Uhusiano wa Karibu Wakati wa Ziara ya Nyanza

Rais William Ruto na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga walihitimisha ziara yao katika eneo la Nyanza wakiwa na mshikamano wa wazi, mavazi yanayofanana, na kushiriki mlo pamoja

Ukaribu wao, kuanzia hotuba hadi vicheko, uliashiria ushirikiano wa kisiasa uliodumu kati ya wanasiasa hao

Nicodemus Mong'are, kiongozi wa vijana na mwanasiasa chipukizi, aliambia TUKO.co.ke kwamba ushirikiano wa Ruto na Raila katika uchaguzi wa 2027 utakuwa wa kutisha

Rais William Ruto na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga walihitimisha kwa pamoja ziara yao ya eneo la Nyanza.

William Ruto na Raila Odinga wapika samaki na kutembea kwenye gati la Homa Bay. Picha: William Ruto.

Chanzo: Facebook

Wanasiasa hao wawili waliunda serikali pana ya umoja, ambapo wanachama watatu wa ODM walipewa nyadhifa kuu serikalini.

Akizungumza katika kaunti ya Homa Bay siku ya Ijumaa, Mei 30, Raila alimtetea Ruto licha ya upinzani dhidi ya ?handisheki? yao.

Raila alisifu serikali hiyo, akisema sasa inatimiza kile alichotarajia alipowania urais mwaka wa 2022.

Raila Odinga na William Ruto wakiwa na mtoto. Picha: William Ruto.

Chanzo: Facebook

Kwa upande wake, Ruto alisema alishirikiana na Raila ili kuleta maendeleo nchini kote. Alisisitiza kuwa hawataruhusu wapinzani kuwavuruga.

Zaidi ya hotuba zao, lugha ya miili yao ilionyesha ukaribu mkubwa, wakionekana kama marafiki wa dhati.

Wote walivaa kofia za jua zenye rangi zinazofanana, pamoja na mashati ya kifahari yenye rangi ang?avu.

Walipozindua makao makuu ya Tarafa ya Rangwe, walihutubia umati wa watu. Raila alikuwa ndani ya gari la Ruto na alizungumza kupitia dari la gari.

Ruto alikuwa amepumzika, hata akaweka mguu mmoja juu ya dari hilo huku Raila akihutubia wananchi.

Rais William Ruto akimsikiliza Raila Odinga akihutubia umati. Picha: William Ruto.

Chanzo: Facebook

Picha nyingine ilionyesha wanasiasa hao wakiwa pamoja na Waziri John Mbadi na Mbunge Peter Kaluma. Raila alionekana kusema jambo la kuchekesha, wote wakishikana mikono na kucheka kwa furaha.

Raila Odinga na William Ruto

Raila Odinga na William Ruto wakishikana mikono Homa Bay. Picha: William Ruto.

Katika soko la kisasa la Homa Bay, Ruto alionyeshwa jinsi ya kuandaa samaki huku Raila akitazama.

Wakati mmoja, Ruto alipika samaki naye Raila akajiandaa kuongeza chumvi.

Raila Odinga na William Ruto wakiwa wameshikana mikono wakiwa Homa Bay. Picha: William Ruto.

Chanzo: Twitter

Nicodemus Mong'are, kiongozi wa vijana na mwanasiasa chipukizi kutoka Eldoret, aliiambia TUKO.co.ke kuwa ushindani wa pamoja wa Ruto-Raila mwaka 2027 utakuwa wa kutisha.

?Issue itakuwa ni nani atawania urais na nani atakuwa wa pili. Uaminifu wa kisiasa hubadilika na hutegemea manufaa ya pande zote. Ikiwa Raila bado ana ndoto ya urais mwaka 2027, inaweza kusababisha kutofautiana.?

William Ruto na Raila Odinga wakitayarisha samaki. Picha: William Ruto.

Chanzo: Facebook

Wakenya walitoa maoni tofauti kuhusu picha hizo:

Faith Amondi: ?Mapenzi ni jambo zuri.?

Josee Wapiwapi: ?Wantam na ndugu yake notam.?

Leakey Omondi: ?Ni miaka kumi bila mapumziko. Rais wa watu na rais wa Kenya. Hii ndiyo picha bora zaidi.?

William Ruto na Raila Odinga wakifurahia samaki. Picha: William Ruto.

Chanzo: Facebook

Samwel Mwangi Njoroge: ?Ndoto ya Raila imetimia ? kuhutubia watu akiwa amesimama juu ya gari la rais. Sasa astaafu kwa amani.?

Eric Kiuru Tosh: ?Tuna furaha kuwaona pamoja. Kenya itanufaika sana kutoka kwa serikali yenu.?

Rodgers Ke: ?Haya ni mapenzi ya kweli.?

Lesiamito Roberts: ?Rais Ruto anaonekana ametulia na mwepesi. Silabasi inasonga haraka.?

Vic Ady Vybz: "Mbinu hii haitafanya kazi ifikapo 2027."

William Ruto na Raila Odinga wakikagua gati ya Homa Bay. Picha: William Ruto.

Chanzo: Facebook

Charlene Ruto aliwakaripia Wakenya

kwingineko, Charlene Ruto alizua mjadala baada ya kuwasihi Wakenya waache kulaumu viongozi kila mara na kuwa raia wenye kuwajibika.

Aliwataka watu kujiuliza kama wanatarajia suluhisho la haraka kwa matatizo magumu na kuhimiza kushiriki kikamilifu katika maendeleo.

Kauli yake ilizua maoni tofauti, wengine wakiiunga mkono huku wengine wakikosoa uongozi anaounga mkono.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke