Jamaa Aliyelimwa Kofi na Pasta Ng'ang'a Kanisani Amtaka Mhubiri Huyo Arudie Kumzaba

Mwinjilisti mashuhuri wa televisheni Mchungaji James Ng?ang?a alikutana na mwanamume ambaye alimpiga kofi hivi majuzi wakati wa ibada ya kanisani

Tukio hilo lilizua chuki za umma, huku wengi wakilitaja kuwa ni shambulio, lakini jamaa huyo alisema hajaudhika na yuko tayari kulishwa kofi tena

Mhubiri alilinganisha tendo hilo na Yesu kutakasa hekalu na kutetea matendo yake

Mchungaji wa kanisa la Neno mwenye utata Mchungaji James Ng'ang'a ameacha ndimi zikitikiswa tena baada ya kuungana na msharika aliyempiga kofi wakati wa ibada.

Kasisi Ng?ang?a aungana tena na mwanamume aliyempiga kanisani. Picha: Sasa TV.

Chanzo: Facebook

Tukio lililosambaa mitandaoni na kuchochea ukosoaji mkubwa

Kwa nini Mchungaji Ng?ang?a alimpiga kofi mshirika wa kanisa?

Katika ibada ya hivi majuzi, mhubiri huyo mwenye utata alimwita mbele mwanaume aliyekuwa amempiga kofi hapo awali kwa madai ya kusinzia wakati wa ibada.

Tukio hilo, ambalo liligusa hisia tofauti kote nchini, lilizungumziwa hadharani kwa mara ya kwanza, ambapo Mchungaji Ng?ang?a na mshirika husika walionekana kutoyumbishwa na lawama zilizotolewa.

?Alinipigia simu lakini sikuwa nimehifadhi nambari yake,? Mchungaji Ng?ang?a aliwaambia waumini.

?Akanipigia tena na nikamwalika kanisani. Baadaye akaniambia, ?Mimi ndiye yule ulinipiga kofi kanisani, Mtume.??

Mchungaji Ng'ang'a alinganisha tukio lake la kumpga jamaa kofi na simulizi la Yesu. Picha: Sasa TV.

Chanzo: Facebook

Mwanaume aliyepigwa kofi na Mchungaji Ng?ang?a azungumza

Kanisa likatulia kimya Mchungaji Ng?ang?a alipomuuliza swali la kushangaza:

?Je, uko tayari kupigwa tena kofi??

Kwa mshangao wa wengi, mwanaume huyo alijibu kwa uthabiti:

?Hakuna shida. Niko tayari kupigwa kofi tena. Acha nipigwe kofi na injili iendelee. Niko tayari kuwa mfano kwa wengine. Huwezi kuwa na mapepo ndani yako halafu uwe na amani. Hilo lilikuwa kofi la baraka.?

Mshirika huyo aliendelea kuelezea jinsi alivyokuwa akisumbuliwa na ndoto za kutisha, ikiwa ni pamoja na visa vya "mke wa kiroho", licha ya kwamba alikuwa akifunga na kuomba milimani.

Kwa mujibu wake, kofi hilo lilimletea mabadiliko ya kiroho.

?Ulishanipiga kofi awali. Ulinipiga kofi lakini haikusambaa. Umenipiga mara mbili. Ilikuwa tamu sana. Ulinipiga kofi nikadondoka ? nilijisikia vizuri,? aliongeza, jambo lililomwacha Mchungaji Ng?ang?a ameduwaa kwa muda.

Ingawa mwanaume huyo alionekana kukubali makofi hayo kama sehemu ya uponyaji wa kiroho, Wakenya wengi kwenye mitandao walilaani vikali kitendo cha mchungaji, wakikitaja kama matumizi mabaya ya mamlaka ya kiroho.

Wataalamu wa sheria na watetezi wa haki za binadamu pia walishangaa ni kwa nini tabia kama hizo zinaendelea kuvumiliwa katika nyumba za ibada.

Licha ya utata huo, Mchungaji Ng?ang?a alibaki bila kujutia kitendo chake, akifananisha matendo yake na Yesu alipofukuza wafanyabiashara hekaluni:

?Nenda ukakae chini,? alimwambia mwanaume huyo.

?Watazamaji wangu, popote mlipo, huyu ndiye yule aliyekuwa amelala. Amerudi. Ukimpenda mtoto, lazima umchape. Bwana yesu alipowakuta watu wakifanya biashara hekaluni ? alibwaga meza zao na kuwatandika viboko.?

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke