Video ya Kutisha Yamuonesha Dereva Akimkanyanga Jamaa Anayeshukiwa Kuchepuka na Mpenziwe na Kumuua

Video ya kutatanisha iliibuka ikimuonyesha mwanamume mmoja akiwa kwenye gari aina ya Ford Ranger akimkanyaga mwingine kimakusudi huko Johannesburg, Afrika Kusini

Mwathiriwa, Emmanuel Mahamba, Mzimbabwe mwenye umri wa miaka 29, alifariki katika eneo la tukio kufuatia shambulio hilo

Tukio hilo linasadikiwa kuwa lilitokana na ugomvi kati ya mwathiriwa na mshukiwa ambao walikuwa wapenzi na mwanamke mmoja

Video ya kuogofya imepepea mitandaoni, ikimuonyesha mwanamume akiendesha gari aina ya Ford Ranger akimkanyaga mwenzake kwenye mitaa ya Johannesburg, Afrika Kusini.

Video ilinasa mwanamume wa Uganda akimkanyaga Emmanuel Mahamba kufuatia kile kinachoemekana mzozo wa mapenzi. Picha: Zim Famous.

Chanzo: UGC

Raia waliripoti kuwa mwathiriwa, ambaye alifariki papo hapo kutokana na kitendo hicho cha kikatili, alikuwa raia wa Zimbabwe kwa jina Emmanuel Mahamba.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 29 alishambuliwa Jumamosi, Aprili 12, karibu saa kumi jioni, kufuatia mabishano na mwanaume kutoka Uganda katika kile kinachoshukiwa kuwa ni mgogoro wa mapenzi unaomhusisha mwanamke aitwaye Ntombizodwa.

Kwa nini mwanaume wa Uganda alimkanyaga Mahamba kwa gari?

Kwa mujibu wa ripoti, mshukiwa, ambaye alitoroka baada ya tukio hilo lililonaswa kwenye video, alikuwa na mtoto na Ntombizodwa.

Pia ilidaiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Mahamba, jambo lililoonekana kuchangia hasira ya mwanaume huyo wa Uganda.

Mgogoro wa mapenzi uliendelea kutokota, na baba wa mtoto wa Ntombizodwa, ambaye sasa ni mshukiwa na yuko mafichoni, alionekana kwa makusudi akimkanyaga Mahamba kwa gari mara kadhaa, na kusababisha kifo chake.

Katika video iliyosambaa mitandaoni, mwanamke mmoja alisikika akipiga mayowe mshukiwa akitekeleza kitendo hicho cha kikatili huku watu wengine wakiwa wamestushwa wakitazama.

Hakukuwa na maafisa wa polisi waliokuwa kwenye tukio hilo katika video, na mshambuliaji alikamilisha mpango wake kisha akaondoka. Mshukiwa huyo alikuwa bado hajakamatwa wakati taarifa hii ilichapishwa.

Raia watoa maoni mitandaoni kuhusu tukio hilo

Gazeti la The Citizen liliripoti kuwa msemaji wa polisi, Kanali Dimakatso Nevhuhulwi, alithibitisha kuwa kesi ya mauaji imefunguliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi, na alihakikishia kuwa uchunguzi unaendelea na hatua za kumtafuta mshukiwa zinaendelea.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii walitoa maoni tofauti, wengi wakilaani kitendo hicho cha kikatili, huku wengine wakielezea madhara ya mahusiano yasiyo na maelewano na usaliti wa kimapenzi.

Baadhi ya maoni ya watumiaji wa mitandao:

Eunnie Wamboi:

?Kwa nini uuwe na uishie jela? Ondoka tu.?

Wilson Gathoga:

?Inaonekana hili lilitokea SA. Hii Ford Ranger ina nambari za GP.?

Agogo Gabu:

?Wake wa watu wengine ? sumu!?

Lyzz Murugi:

?Alikuwa mpenzi wa pembeni kwa wote wawili. Muganda aligundua hatathaminiwa. Lakini hili ni la kusikitisha sana.?

Annielito Lito:

?Badala ya kuchiti, kwa nini usiondoke uende na yule unayempenda zaidi??

Oliver Wafula Sifuna:

?Ni nani wa kulaumiwa??

Ojiambo Ainea:

?Mwanaume ataishia jela, na mwanamke ataendelea kuchepuka.?

Christine Atieno Otieno:

?Kwa nini mtu aangamize maisha yake kwa njia ya kijinga namna hii? Watu ni wajinga kiasi gani??

Osiemo Edwin:

?Kama mwanaume, ukigundua mpenzi wako amekusaliti, jambo bora zaidi ni kuondoka kwa ajili ya ustawi wako.?

Vanessa Struwig:

?Kwanini hata hakujaribu kumsaidia??

Favor Mutheu Muumba:

?Badala ya kupiga mayowe, kwa nini usimvute kando kuokoa maisha? Kelele hazisaidii. Nathamini maisha sana, na hakuna anayestahili kupoteza maisha kwa njia kama hiyo.?

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke