William Ruto Asema Mwanawe Anasomea Usimamizi wa Michezo Nje ya Nchi: "Kusaidia Harambee Stars"

Rais William Ruto alifichua kuwa mmoja wa wanawe anasomea shahada ya uzamili katika usimamizi wa michezo

Alishiriki habari hizo alipokuwa akiitangaza timu ya soka ya Kenya ya U-20, Rising Stars, kabla ya michuano yao ya AFCON nchini Misri

Ruto alisema mwanawe anapenda masuala ya soka na anatumai kuchangia ukuaji wa michezo nchini

Rais William Ruto hivi majuzi alishiriki kuhusu mapenzi ya mwanawe kwa michezo.

Rais William Ruto alisema mmoja wa wanawe anapenda maswala ya michezo. Picha: William Ruto.

Chanzo: Facebook

Rais Ruto aliwaalika wachezaji wa timu ya Rising Stars katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumanne, Aprili 15.

Ruto aliwaaga rasmi vijana hao wa chini ya miaka 20 waliokuwa wakielekea kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.

Timu hiyo itacheza mechi yao ya kwanza dhidi ya Morocco mnamo Mei 1.

?Niko nyuma yenu kama nilivyosema, na tafadhali nifanyeni nije kwenye fainali za AFCON. Nitakuwepo,? aliahidi.

Ruto alifichua kuwa mmoja wa wanawe ni mpenzi mkubwa wa soka na humsihi mara kwa mara aboreshe hali ya michezo humu nchini.

?Mwanangu ni shabiki mkubwa wa soka, na kila mara hunambia kuwa tunapaswa kufanya kitu kuhusu michezo.?

Mwanasiasa huyo alisema kuwa mwanawe huyo anasomea usimamizi wa michezo (sports management) kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya michezo nchini Kenya.

?Na ili mjue jinsi alivyo na dhamira, ameenda kusomea shahada ya uzamili katika usimamizi wa michezo kwa sababu anataka kuja kuwasaidia. Vijana wa Kenya wanaona fursa na uwezo ulioko katika michezo.?

Tovuti ya TUKO.co.ke ilibaini kuwa mtoto anayezungumziwa ni George, mwana mdogo wa Ruto.

?Alianza kusomea shahada hiyo ya uzamili miezi michache iliyopita jijini London, Uingereza,? chanzo kimoja kilisema.

Wakenya wengine walisifu hatua hiyo, huku wengine wakieleza wasiwasi kwamba huenda rais akampa mwanawe kazi serikalini baada ya kumaliza masomo.

Baadhi ya maoni ya Wakenya ni haya:

bramuel.io:

?Mwaka ujao mtamwona akiwa Waziri wa Michezo.?

_ndindam:

?Ili uje umpe kazi? Tuko macho.?

jeff.ason.:

?Wangapi tayari wamesoma sports management hapa Kenya??

maigo_dennis:

?Na watu wanapiga makofi.?

Kevinkendrickid:

?Michezo itabadilika hivi karibuni Kenya.?

wambuiliz322:

?Anaandaliwa kuingia serikalini.?

sir___elliott:

?Unamaanisha hakuna mwingine mwenye shahada ya usimamizi wa michezo anayeweza kusimamia sekta hii??

eric_labznopy:

?Sisemi chochote, lakini najua ningesema nini. Ni woga tu unaniondoa.?

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke