Aliyekuwa Afisa wa KDF Asimulia jinsi Madai Kwamba Anachepuka na Bosi Yalifanya Afutwe Kazi

Zipporah Kata alikuwa amepandishwa cheo hadi koplo alipohamishwa hadi kituo kingine

Mkubwa wake inadaiwa alitaka uhusiano wa kimapenzi naye, na alikubali licha ya kutokuwa na wazo hilo

Uhusiano wao unaodaiwa ulifikia kikomo baada ya miezi saba, pale ambapo Zipporah kutoka Ongata Rongai alipatikana na risasi nyumbani kwake

Mama huyo wa watoto wawili aliambia TUKO.co.ke kwamba afisa wake mkuu alidaiwa kutega risasi hizo nyumbani kwake alipokuwa hayupo

Mwanamke kutoka Ongata Rongai, kaunti ya Kajiado, amefunguka kwa huzuni jinsi alivyopoteza kazi yake ya ndoto.

Aliyekuwa afisa wa KDF Zipporah Kata afunguka kuhusu uhusiano wa kimapenzi na afisa mkuu. Picha: TUKO.co.ke/Kelvin Starbizzy.

Chanzo: Original

Zipporah Kata anaripotiwa kushiriki katika uhusiano wa kimapenzi na bosi wake wa ngazi ya juu, jambo ambalo anadai baadaye alilipia kwa gharama kubwa na kwa majuto.

Kwa mujibu wa Kamusi ya Cambridge, ni kitendo cha kukutana na mtu kijamii, hasa mtu kutoka jeshi pinzani au timu tofauti, au mwenye nafasi ya kijamii tofauti na yako.

Akizungumza na TUKO.co.ke, Zipporah, mama wa wasichana wawili warembo, alidai kuwa uhusiano wa kimapenzi na afisa wake wa juu ulimgharimu kazi yake.

?Nilipandishwa cheo kutoka private wa ngazi ya juu hadi kuwa corporal baada ya kumaliza masomo yangu kambini. Nilihamishwa kituo hadi Defence Staff College. Nilipofika huko, yule bosi niliyempata alianza kunikaribia kimapenzi. Niliambiwa nitakuwa namhudumia chai na kushughulikia chakula chake, jambo ambalo sikuwa nalipenda. Kutokana na hiyo kazi, tulikuwa tunakutana mara kwa mara. Uhusiano huo uliendelea kuanzia Mei 2019 hadi Novemba 2019,? alieleza.

Zipporah alikuwa anafanya nini Isiolo?

Kabla ya uhusiano wao kuharibika, Zipporah alikuwa amejiunga na kikosi cha Six Brigades, kikosi cha kijeshi kilichokuwa kinajiandaa kupelekwa Somalia.

Alipitia mafunzo ya kupelekwa uwanjani huko Isiolo kwa muda wa miezi mitatu ili kumwandaa kwa majukumu ya kijeshi Somalia.

?Kabla miezi mitatu kuisha, tulipeleka mizigo yetu Garissa, kisha tukarudi kuwaaga familia zetu kabla ya kwenda Somalia. Nilipofika Ijumaa, nilipokea simu kutoka kwa namba isiyojulikana. Alijitambulisha kama afisa wa polisi wa kijeshi na kuniambia kuwa walikuwa wametumwa kupekua nyumba yangu.

?Baada ya kunijulisha hivyo, nilijiandaa na kwenda ofisini kwao ili kuwarudisha kwangu. Walipofika, walipata risasi ndani ya nyumba. Lakini ni kama bosi wangu alikuwa tayari amewaarifu kuhusu hizo risasi, kwa sababu walikuwa tu wakinichezea akili. Ndipo nikapoteza kazi yangu,? alidai.

Zipporah alifanya kazi KDF kwa muda gani?

Mama huyo wa watoto wawili alisema bosi wake alimwekea risasi hizo nyumbani kwa nia ya kumfukuza kazi.

Alisema mdosi huyo alikuwa na funguo za nyumba yake ya chumba kimoja, na alikuwa akiingia humo alipokuwa hayupo.

?Tuliwahi kugombana na bosi wangu, na alinitishia kuwa sitakwenda Somalia. Nilidhani alikuwa anatania hadi haya yaliponitokea. Nilipoteza kazi yangu baada ya miaka 11, siku 138,? alieleza kwa masikitiko.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke