Lofa Achanganyikiwa Kupata Mpenzi Amefagia Nyumba,Amehepa na KSh 240k: "Ameniwachia Ndoo Moja"

Philion Bulegeya hajui ataanzaje baada ya kurudi nyumbani na kupata mke amebeba kila kitu nyumbani na kuondoka

Bulegeya alishuku kuwa mke wake wa miaka miwili alitoroka na vitu vya nyumbani, akamwacha na vitu vichache

Mwanamume huyo Mtanzania pia alibaini kuwa mkewe alitoweka na akiba yao ya KSh 240,000, walizopanga kuzitumia kujenga nyumba

Kijana mmoja kutoka Kigoma, Tanzania, amevunjika moyo baada ya kukaribishwa na mapokezi ya kuhuzunisha nyumbani kwake.

Kijana wa Kitanzania Philion Bulegeya akiwa amekaa chini. Picha: Ayo TV.

Chanzo: Youtube

Philion Bulegeya karibu atokwe na machozi baada ya kurejea nyumbani na kukuta nyumba ikiwa tupu, kila kitu kimechukuliwa.

Hakuweza kumpata mke wake wala mali zao, isipokuwa vitu vichache alivyomuachia.

Bulegeya alikutana vipi na mke wake?

Bulegeya alisimulia siku aliyokutana na mke wake na jinsi walivyokuwa marafiki wa karibu kabla ya kuoana.

"Nilikuwa kwenye basi tulipokutana kwa mara ya kwanza. Tulibadilishana nambari za simu na tukaanza kuzungumza. Alikuwa mnyenyekevu na mtiifu. Alikuwa na sifa zote za kuitwa mke. Tulifunga ndoa mwaka wa 2023," alisema Bulegeya.

Alikiri kuwa uhusiano wao haukuwa tofauti na mingine ambapo ugomvi wa hapa na pale hujitokeza.

Hata hivyo, alikanusha kuwepo kwa mzozo mkubwa uliowahi kuwalazimu kutafuta msaada wa watu wa tatu.

Bulegeya afunguka kuhusu ugomvi na mkewe

"Tuligombana, bila shaka. Kulikuwa na nyakati nzuri na ngumu, lakini hatukuwa na mzozo mkubwa hadi tukaitisha usuluhishi wa wazazi wetu. Tulitatua changamoto zetu sisi wenyewe. Hajawahi kurudi kwao kwa sababu ya ugomvi. Mizozo yetu ilikuwa midogo tu," aliongeza.

Pamoja na hayo yote, Bulegeya alimshtumu mke wake kwa kuiba mali zote za nyumbani na kutoroka nazo, ikiwemo pesa taslimu KSh 240,000.

Juhudi za kumfikia mkewe kwa simu hazikufaulu kwani simu yake imekuwa ikizimwa tangu alipotoweka.

"Nimejaribu kumpigia simu mara kadhaa. Nilipofika nyumbani na kutomkuta, nilijaribu kumpata kwa simu lakini haikupatikana. Nilikwenda kituo cha polisi kuripoti kutoweka kwake pamoja na mali ya nyumba, kisha nikawaarifu jamaa zake. Niliwauliza majirani na marafiki wake kama wanajua alikoenda, lakini sikupata jibu," aliongeza.

Onyo la Bulegeya kwa wapenzi

Bulegeya alisema tukio hilo limemrudisha mwanzo kabisa, akilazimika kuanza upya baada ya kuachwa bila chochote.

Alibaki na ndoo moja tu aliyomuachia mke wake, na kwa kuwa kitanda chao cha sita kwa sita kilikuwa kimechukuliwa, alilazimika kulala kwenye mkeka.

Alitoa ushauri kwa wapenzi kuwa waangalifu wanapochumbiana kabla ya kuingia kwenye ndoa, baada ya kupitia masaibu hayo miaka miwili tu ndani ya ndoa.

Bulegeya aliwaonya watu wasikimbilie mapenzi bila kujua vizuri watu wanaowapenda na kujitolea kwao, la sivyo wapate masaibu kama yake.

Nyumba ambayo Philion Bulegeya na mkewe walikuwa wakiishi Tanzania. Picha: Ayo TV.

Chanzo: Youtube

Mwanaume wa Murang?a aachwa bila kitu baada ya miaka 20

Katika kisa kama hicho hapa nyumbani, mwanaume mmoja kutoka kaunti ya Murang?a aliachwa bila chochote baada ya mke wake kutoweka na mali yote ya nyumbani.

Kabla ya mkewe kutoroka, Peter Karanja alikuwa amegundua siri chafu za mkewe zilizomuumiza sana.

Mkewe alikuwa anaendesha biashara haramu, na biashara hiyo ilipoanguka, alitoroka na mali yote ya familia.

Kama hilo halikutosha, Karanja aliambia TUKO.co.ke kuwa mke wake aliuza mifugo yao na kubomoa baadhi ya majengo yao.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke