Kasisi wa Kikatoliki wa Kisii Azua Mjadala kwa Kuwafukuza Washarika Waliokuwa Wamevalia Vibaya
Padre Benjamin Ndemo kutoka Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro na Paulo huko Mugirango Kusini, Kisii anadaiwa kuwafukuza waumini kwa sababu ya mavazi yasiyofaa
Vitendo vyake vilivutia sifa mtandaoni kutoka kwa baadhi ya Wakenya waliodai kuwa watu wengi wamekengeuka kutoka kwa mapenzi ya Mungu
Wakenya wengine walidai kuwa kasisi huyo alikuwa sahihi kulinda utakatifu wa kanisa na kuwataka waumini wenzake kuvaa kila mara kwa heshima
Kisii - Kasisi mmoja katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro na Paulo huko Mugirango Kusini, Kisii, amezua mjadala mtandaoni baada ya kuripotiwa kuwanyima waumini nafasi ya kusikiliza ibada.
Kuhani akisubiri ishara kanisani (Picha kwa kielelezo). Kisa hicho kilitokea Kisii. Picha: FangXiaNuo.
Chanzo: Getty Images
Jinsi Wakenya Walivyoitikia Hatua ya Padre Ndemo
Vivaton Vivacx alisema:
"Ingawa mimi si Mkatoliki, namuunga mkono huyu padri. Lazima tujifunze tofauti kati ya kanisa na klabu."
Fredie Kouko alihimiza:
"Acha hii iendelee katika makanisa yetu kote Kenya. Ienee kama moto. Si wanawake tu bali hata wanaume wanaovaa suruali za kubana wapitie hali hiyo. Baadhi ya suruali hizi zinakaa vibaya sana. Hata mitindo ya nywele isiyo ya heshima kwa mtu anayemcha Mungu haifai. Mavazi ya heshima kwa kila mtu."
Diboo The Blogger alisema:
"Namuunga mkono padri kikamilifu. Nguo za kubana, sketi fupi, na blauzi za kuanika vitumbo ni za aibu."
John Bosco Trees alishauri:
"Alikuwa sawa kabisa. Ni kuhusu mafundisho na yeye ndiye anayewajibika kuhakikisha viwango vinazingatiwa. Yeyote anayehisi kuumizwa anaweza kuchukua hatua inayofaa kwake."
Mbedha Julius alisema:
"Huo ni uamuzi wa busara, Mchungaji. Je, unaweza vipi kumtarajia mtu asiyeweza kuheshimu hekalu la Mungu, ambalo ni mwili wake, atamuheshimu Bwana katika nyumba yake? 1 Timotheo 2:9; 1 Petro 3:3-5."
Sharon Dezy alijibu:
"Wamama sione maoni kwenu. Kwa vyovyote vile, ni vizuri kuvaa kiheshima ukienda kanisani. Tunapaswa kuheshimu nyumba ya Mungu."
Tonick Ojero alisema:
"Tunapaswa kuvaa kwa heshima. Miili yetu ni hekalu la Bwana. Ninasifai kanisa kwa kazi nzuri."
Korwa Orwa alisema:
"Hii ni hatua nzuri sana. Tunahitaji kuonyesha heshima katika nyumba ya Bwana."
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke